Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. KANGI A. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa, nina dakika tano tu, nianze na maneno haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2023/2024 tulianzisha mradi wa vijiji 24 Jimbo la Mwibara na tukatenga token ya shilingi 741,800,243. Mradi huo unahusu vijiji 24 vya Kisorya, Nambubi, Nampangala, Masahunga, Bwanza, Nansimo, Makwa, Busambu, Sunsi, Mwitende, Nambaza, Bunere, Busambara, Igundu, Bulendabufwe, Namalebe, Mchigondo, Namalama, Kitengule, Kibara A, Kibara B, Kibara Stoo, Mwibara na Nakatuba, lakini kwa bahati mbaya fedha hazikupatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukaja mwaka wa fedha 2024/2025 tukatenga fedha shilingi bilioni moja kama token, lakini fedha hazikupatikana, mwaka wa fedha 2023/2024 tukatenga fedha, lakini fedha hazikupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Maji, Mheshimiwa Aweso anafanya kazi kubwa sana kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Watanzania tunapata maji, lakini kinachomwangusha ni tatizo la fedha. Tutapiga kelele, tutaomba miradi, lakini hakuna fedha. Sasa tukiendelea kutegemea fedha hizi za ndani, ninaamini vijiji hivi 24 vya Mwibara havitapata maji. Ninaomba, tutafute kwenye alternative financing ili tupate fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila mwaka wa fedha tunatenga fedha, tunasema mradi utatekelezwa na hautekelezwi. Tutafika mahali hatutaaminika. Wana Mwibara wasipomwamini Mbunge kwa yale anayoyasemea wataenda mbali zaidi, watailaumu Serikali. Sasa kama shida ni upatikanaji wa fedha, na kwa nguvu zake zote imeshindikana, labda nishauri kama kanuni zinaruhusu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua wakati mwingine tukimtegemea Mungu anaweza akajibu. Kama Kanuni zinaruhusu nije hapo mbele ashike bajeti yake nimwombee kwa Mungu ili Mungu aweze kujibu, kwa sababu haiwezekani miaka yote hii ya fedha tunatenga fedha hazipatikani! Tunatenga fedha hazipatikani! Tunatenga fedha hazipatikani, lakini kwenye maombi kila siku tukicha wenzetu Makanisani na Misikitini aah, maombi hujibiwa na matokeo tunayaona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme mambo mawili ya muhimu sana. Jimbo la Mwibara tumezungukwa na maji na kijiji cha mwisho ni kilometa mbili kutoka kwenye chanzo cha maji ya Ziwa Victoria. Kijiji ambacho kipo mbali na maji, kiko kilometa mbili, inakuwaje badala ya kusubiri tupate fedha hizi nyingi, tunaweza…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa malizia, muda wako umeisha, malizia kengele ni moja tu.

MHE. KANGI A. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja. (Makofi)