Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon Silvery Luboja Salvatory

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. SILVERY L. SALVATORY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi hii. Awali ya yote, ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai. Pia ninawashukuru watendaji wa Wizara ya Maji wakiongozwa na Mheshimiwa Waziri Aweso, pia nisimsahau Meneja wangu wa RUWASA, ndugu yangu Mapengo kwa kazi nzuri ambazo amekuwa akizifanya kwenye Jimbo la Misungwi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa faida ya muda, ninaomba nitambue juhudi kubwa za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na niseme tu kwamba zimeainishwa kwenye ukurasa…

(Hapa haikusikika kutokana na hitilafu ya kipaza sauti)

MHE. SILVERY L. SALVATORY: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sasa barabara zifuatazo, Wizara ya Maji ikashirikiane na Wizara ya Ujenzi na mamlaka nyingine za Serikali ili waone na zenyewe zinafanyiwa usanifu wa kina ili ziweze kufanya operation nzuri kwenye mradi wa maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo Barabara ya kutoka Buhingo Nyamainza – Ihelele ina urefu wa kilometa 30, ambayo inatoka Mwanangwa inakuja kuunga kwenye hiyo junction. Tunayo Barabara ya Manawa – Kasololo – Mbarika, ina urefu wa kilometa 38.5 ambayo wakati wa masika ziwa huwa linajaa linaziba njia. Kwa hiyo, ninaomba kama tuna nia ya dhati ya hiyo Gridi ya Taifa, tukaweze kuizingatia hiyo barabara na kuihudumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo Barabara ya kutoka Mbarika – Ilujamate – Nhundulu yenye urefu wa kilometa 46.6. Ninaomba hayo yazingatiwe na ninarudia kuishukuru Wizara ya Maji na watendaji wake wote kwa hotuba nzuri na kwa kuainisha miradi yote kama ambavyo imeonekana kwenye ukurasa wa 266 – 268 kwenye Jimbo langu la Misungwi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ninaunga mkono hoja. (Makofi)