Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkenge
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi ya kuchangia Wizara ya Maji. Ninasema leo sikutaka kuchangia Wizara hii, lakini imebidi nisimame kutoa ushuhuda wa kazi nzuri ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ushuhuda wa ndugu yangu Waziri Aweso, ambaye amekuwa kwenye Wizara hii akihudumu vizuri pamoja na wasaidizi wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo matatu. Kwa ufupi nitatoa ushuhuda, nitaomba, lakini mwisho nitashauri. Pongezi za kwanza za dhati ziende kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunaona nia yake ya dhati ya kubadilisha wananchi wake ndani ya Tanzania kwa kuhakikisha kwamba, kila mmoja anapata maji. Hii inakuwa reflected kwenye bajeti, kutoka bajeti iliyopita ya shilingi 898,000,000,000 na leo tunaenda kwenye shilingi 1.12 trillion, kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji. Ni pongezi kubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawapongeza viongozi waandamizi wanaomsaidia Mheshimiwa Rais; Mheshimiwa Dkt. Balozi Emmanuel Nchimbi pamoja na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kwa kuendelea kumshauri Mheshimiwa Rais vizuri. Pongezi za dhati ziende kwa askari wake wa mwanvuli, ambaye ni Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso, Ndugu yangu Mheshimiwa Engineer Kundo, pamoja na wasaidizi wao, wakiwa na Mtendaji Mkuu, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, lakini na viongozi wa Taasisi ya RUWASA, bila kumsahau Ndugu yangu Engineer Krita na Wakurugenzi wote wa Wizara hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye mikoa yetu tunaona tunao wasaidizi wao, wanafanya kazi kubwa na kwa ueledi. Kwa Mkoa wa Kagera tunaye ndugu yangu Warioba Sanya, lakini kwenye wilaya yangu tunaye Engineer Robert, ambao wanaendelea kufanya kazi pamoja na watumishi wengine wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema Wilaya ya Misenyi inasimamiwa na taasisi mbili, chini ya Mheshimiwa Waziri Aweso; pamoja na RUWASA tunayo BUWASA. BUWASA yenyewe inaendelea kufanya kazi nzuri chini ya Ndugu yangu John Slatt, ambaye ni Mkurugenzi na kijana wake Mheshimiwa Aweso, ambaye ni Engineer Lucas Mbaga ndani ya Wilaya ya Misenyi, anafanya kazi nzuri kusimamia Mradi mkubwa wa Maji kutoka Chaka – Bunazi mpaka Kasambya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushuhuda wangu wa kwanza ni, katika historia tangu nchi imeumbwa Wilaya ya Misenyi, kata 15 zilikuwa hazina maji, lakini ndani ya kipindi cha miaka mitano kwa ushuhuda huu, ndani ya Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso, kata 15 sasa zina maji. Maji yanaendelea kusambaa na wananchi wangu wa Wilaya ya Misenyi waendelee kuvumilia, yale maeneo machache ambayo maji hayajafika katika hizo kata 15 yataendelea kusambazwa kwa sababu, jumuiya za watumia maji zinaendelea kufanya kazi nzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, basi ninaomba, Mheshimiwa Hamidu Aweso, katika kata tano zilizobaki; Kata ya Minziro, Kata ya Bugorora, Kata ya Bugandika, Kata ya Bwanja na Kata ya Kakunyu, tuimarishe. Tuhakikishe na zenyewe sasa zinapata maji safi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushuhuda wangu wa pili ni vyanzo vya maji ndani ya Wilaya ya Missenyi. Missenyi tumebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji, tunalo Ziwa Victoria ambalo linazunguka Wilaya ya Missenyi, tunao Mto Kagera na Mto Ngono. Hii yote ilikuwa haijawahi kutumika kwa hiyo, sasa tunaona historia imeandikwa, kote maji yamefika kutoka vyanzo hivyo. Namwomba sasa, Mheshimiwa Aweso, ndani ya wilaya yetu maeneo yaliyobaki yote miradi ifike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Eneo la Mtukula kuna Mradi mkubwa wa BUWASA, mkandarasi anadai fedha, mradi uko 70%. Ninaomba alipwe shilingi 929,000,000 amalizie, lakini ninakushukuru kwa fedha shilingi milioni 200 maeneo ya Bwengabo, Biyawala, Kagarama, Kashaba mpaka Buliyambo Kona, fedha zimefika tunaendelea kuzitumia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi na ninaunga mkono hoja. (Makofi)