Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Ninaomba nimpongeze sana Waziri kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya pamoja na Naibu Waziri, pamoja na Katibu Mkuu na Management yote ya Wizara, pamoja na viongozi wote wanaosimamia mamlaka ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, RUWASA ndiyo inafanya kazi vijijini. Tulikuwa tunaomba RUWASA ipewe kipaumbele, kwa sababu ndiyo inashughulika na miradi yote ya vijijini, kuhakikisha wanawake wa vijijini wanapata maji safi na salama. Ninaomba nimpongeze Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Kirita, kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kusimamia mamlaka zote za mikoa, ma-RM wote, kwa ajili ya kuhakikisha miradi inakwenda vizuri. Ninaomba RUWASA, ma-RM hawana OC ya kwenda kuhakikisha kufuatilia miradi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba RUWASA iongezewe bajeti na isimamiwe vizuri ili miradi ile ya vijijini iweze kwenda kusimamiwa vizuri. Ma-RM, ma-MDs wanafanya kazi vizuri katika maeneo yetu. Ili tuweze kufanya kazi vizuri, Mfuko wa Maji lazima uongezewe pesa. Mfuko wa Maji ndiyo utafanya kazi vizuri kuhakikisha nchi yetu inakwenda vizuri, maji yanapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimpongeze Mkurugenzi Mkuu, Haji kwa kazi kubwa ambayo anausimamia Mfuko wa Maji kuhakikisha pesa zinapatikana. Serikali nayo ihakikishe inaongeza pesa kwenye Mfuko wa Maji ili maji yaweze kupatikana katika maeneo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna miradi mbalimbali katika maeneo yetu, ndiyo maana nimesema RUWASA na Mfuko wa Maji waongezewe bajeti kwa sababu kuna miradi sasa hivi imesimama. Jimbo la Nsimbo, kuna Mradi wa Ivungwe, kuna Mradi wa Tumaini, kuna Mradi wa Kabuga, yote imesimama kwa sababu wakandarasi hawajapata pesa zao. Ninajua Serikali ina malengo mazuri, lakini tukiweza kuweka nguvu kwa RUWASA wakapewa bajeti nzuri na Mfuko wa Maji ukapewa bajeti nzuri, hawa wakandarasi wote hatutaweza kupata nao tabu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu tunakwenda haraka, katika Jimbo langu la Nsimbo, Halmashauri ya Nsimbo, nina Kata pale za Mtapenda, Kapalala, Nsimbo yenyewe pamoja na Urwila, pamoja na vijiji vyake. Tunahitaji mradi mwingine mpya, Mradi wa Ikolongo, kwa sababu watu wameongezeka na vilevile ni Makao Makuu ya Halmashauri yetu ya Nsimbo, kuna Hospitali ya Wilaya, kuna mambo mengi katika halmashauri ya Nsimbo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Mheshimiwa Aweso, ninajua ni msikivu, nimpongeze sana, kwa sababu amefika katika maeneo yale. Alikuja katika Kijiji cha Mtakuja, alikuja katika Kijiji cha Songambele, alikuja katika Kijiji cha Isinde, unajua adha ya wananchi, maji bado hayatoshelezi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Mheshimiwa Waziri, Aweso, yeye ni msikivu. Tunampenda, tunaomba maji, Mradi wa Ikolongo uanze mara moja, ili kuweza kuondoa adha ya Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo, Halmashauri ya Nsimbo pamoja na wananchi, hususan Kijiji cha Kapalala, hakina maji kabisa. Ninajua alifanya jitihada kubwa, alipeleka gari mara mbili, ninaomba nimpongeze RM wa Mkoa wa Katavi, Iddi Pazi, alipeleka gari mara mbili kuhakikisha kuchimba visima, lakini maji hayakupatikana. Tukianzisha mradi huu wa Ikolongo, ninafikiri vijiji vyote, vya kata zote, watapata maji safi na salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa, wametuletea pesa, miradi inaonekana, wananchi wanapata maji safi na salama. Hiyo ni kazi kubwa ambayo amefanya Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuwatua ndoo kichwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, viongozi wote wa Wizara, Engineer Mwajuma amefanya kazi kubwa na nzuri. Amejitahidi kuhakikisha wanawake anawachimbia visima. Ninaomba nimpongeze Katibu Mkuu pamoja na management yake yote kwa kazi kubwa na ufuatiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niunge mkono hoja kwa kazi kubwa na nzuri ya Wizara ya Maji. Ahsante sana. (Makofi)