Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kivule
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. DOUGRAS D. MASSABURI: Mheshimiwa Spika, nami nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema. Leo nimepata nafasi kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kivule kuongea masuala yanahusu maji ndani ya Jimbo letu la Kivule.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwanadiplomasia nguli, mara ya mwisho niliposema Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, humu ndani ni mwanadiplomasia nguli, wako watu walibeza kauli zile kwenye vyombo vya habari, lakini leo wameuthibitishia umma na dunia, Tanzania na Bara la Afrika kwa kumteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Upinzani kuwa kwanza si tu Mheshimiwa Mbunge, lakini pili Naibu Waziri wa Kazi Ajira na Mahusiano. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan oyeee. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kiongozi anaye kwenye siasa za kujenga, ni kiongozi anayeamini kwenye hoja mbadala; ni kiongozi aliyevuka mipaka ya kisiasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan sisi wananchi wa Jimbo la Kivule wakati anaingia madarakani, kwa takwimu za watu wa SINOVET mwaka 2008, Jimbo la Kivule lilikuwa na maji 0%, lakini leo miaka 15 baadaye Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amejenga tenki kubwa la maji la lita 9,000,000 pale pale Pugu Bangulo na maji yale yanatiririka kwenda kwenye Majimbo ya Segerea, Jimbo la Ukonga na Jimbo letu jipya la Kivule na hivyo kufanya Jimbo la Kivule kuwa na maji sasa 48%. Kati ya kata sita tayari kata tatu zimekwishapata maji safi na salama. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, katika muktadha huo ninayo heshima kubwa kumshukuru kaka yangu Mheshimiwa Jumaa Aweso, mtoto wa Fatma Omari Masanga, mtoto wa mamalishe, anayefahamu nini shida ya maji, alikuja ndani ya Jimbo la Kivule, akakutana na mamalishe, babalishe, wauza mboga mboga akaahidi kuchimba visima 10. Kati ya mitaa 29 tayari visima vitatu vimekwishaanzachimbwa na viwili vimekwishaanza kutoa maji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninampongeza sana kaka yangu Mheshimiwa Aweso na management yote kwa ujumla wake akiwemo dada yetu Katibu Mkuu, dada yetu Injinia Mwajuma. Pia nimpongeze sana kaka yangu Bwire na watu wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa namna ambavyo wamekuwa wakifanya kazi ya maji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nijikite kwenye ushauri wakati ninamsikiliza ndugu yangu Mheshimiwa Aweso, jana aliishia na maneno mawili alisema anataka Taifa lenye uhakika wa maji na akasema nataka kuwe na wizara ya kuchochea uchumi wa Taifa.
Mheshimiwa Spika, ninapenda nimwambie ninaunga mkono kazi kubwa anayoifanya, lakini namtaka ajifunge mkanda yeye na watu wote kwenye Wizara ya Maji inatupaswa tuwe na total turn around watu wote waliosimama kwenye Bunge hili Tukufu kila mmoja amezungumzia upotevu wa maji mahitaji ya maji Mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya lita milioni 700,000.
Mheshimiwa Spika, mahitaji maji yanayotengenezwa ni zaidi ya lita 500,000,000 yanayopotea ni lita 250,000,000 ukiya-quantify ni zaidi ya shilingi 138,000,000,000. Fedha hizi tungeweza kuziokoa zingeweza kujenga vituo vya afya, zingeweza kujenga barabara za Kivule, zingeweza kuleta madawa na zingeweza kujenga mabwawa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali umetuambia kwamba 70% itokane na alternative financing. Nami ninaishauri Serikali yangu kama kuna mahali ambako Serikali na sekta binafsi wanaweza kuwa na interest ya kuwekeza wasisite kufanya hivyo. Unapowekeza kupitia sekta binafsi unaokoa kodi za Watanzania, unapookoa kodi za Watanzania unali-allocate pesa kwenda kwenye maeneo muhimu na mtambuka kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, hivyo niombe sana na nitashika shilingi siku ya mwisho kwenye bajeti yetu ya mwisho kwenye kitengo cha PPP. Tumekubaliana 70% itokane na sekta binafsi, lakini bado kitengo cha PPP hakijapewa muscles ya kutosha kwa maana ya bajeti tulioisikia kwenye Wizara ya Mipango na Uwekezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninaomba niunge mkono hoja lakini nimtie moyo kaka yangu Mheshimiwa Jumaa Aweso kwa kazi kubwa anayoifanya. Mwenyezi Mungu ambariki, wananchi wa Kivule wanamshukuru na kumpongeza na kumkaribisha wakati wote katika mapambano ya kuwatafuta maji na kumtua mama ndoo ya maji kichwani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninaomba niunge mkono hoja na ahsante kwa kunisikiliza. (Makofi)