Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Janeth Peter Pinda (1 total)

MHE. JANETH P. PINDA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya kutoka Wilaya ya Tanganyika hadi Uvinza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Peter Pinda, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa barabara hii unatekelezwa kwa awamu ambapo ujenzi kwa sehemu ya kwanza ya Mpanda – Vikonge kilomita 37.65 umekamilika. Ujenzi wa sehemu ya pili ya Vikonge – Luhafwe kilomita 25 unaendelea na umefikia 70% na ujenzi wa sehemu ya tatu ya Luhafwe – Mishamo kilomita 37.35 unaendelea na umefikia 30.6%. Kwa sehemu iliyobaki ya Mishamo – Uvinza urefu kilomita 95.6, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.