Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Haiderali Hussein Gulamali (2 total)

MHE. HAIDERALI H. GULAMALI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Ninataka kujua, ni lini Hospitali ya Manispaa ya Mpanda itapata jengo la emergency?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimejibu kwenye majibu ya awali, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Hospitali ya Mpanda nayo imo katika mpango wa zile hospitali 105 ambazo tumeshatenga bajeti katika mwaka wa fedha 2026/2027, jumla ya shilingi bilioni 52.25, ambazo tutazielekeza katika kukamilisha baadhi ya miundombinu muhimu.

Mheshimiwa Spika, ni kweli jengo la emergency ni muhimu sana kwa sababu linatoa huduma kwa wakati na baadhi ya wagonjwa huishia tu kutibiwa emergency na kwenda nyumbani. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa jengo hili muhimu.
MHE. HAIDERALI H. GULAMALI: Mheshimiwa Naibu Spika, tumkumbushe Mheshimiwa Waziri kwamba, pale Ilongero shule zetu zina uchakavu mkubwa sana, zinatakiwa ukarabati katika kata mbalimbali. Tuliwasilisha maombi yetu kwa maandishi ofisini kwa Mheshimiwa Waziri. Tunaomba majibu.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninawapongeza wananchi wa Jimbo la Ilongero pamoja na Mheshimiwa Mbunge kwa kuwasilisha orodha ya shule ambazo ni chakavu na zinahitaji ukarabati. Ninaomba nimhakikishie kwamba, Serikali inaandaa mpango mkakati mahususi ambao utaainisha shule zote chakavu ambazo tayari, of course tumeainisha, lakini tunatafuta fedha kwa ajili ya kuona namna ambavyo tutakwenda kuzikarabati shule zile kwa awamu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie kwamba katika vipaumbele ambavyo vipo kwenye sekta ya elimu ni pamoja na kwenda kuondokana na shule chakavu na kongwe. Tunaendelea na taratibu za kupata fedha, ili tuje kukarabati. Tutahakikisha kwamba shule za Jimbo la Ilongero pia zitapata kipaumbele.