Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Edwin Enosy Swalle (1 total)

MHE. EDWIN E. SWALLE aliuliza:-

Je, lini Serikali itarejesha Kiwanda cha Chai cha Wakulima wa Chai Lupembe (MUVYULU)?
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, ninaomba nijibu swali namba 142 kama lilivyoulizwa na Mheshimiwa Edwin Enosy Swalle, Mbunge wa Lupembe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda cha Lupembe Tea Factory kilichopo wilaya ya Lupembe kilibinafsishwa mwaka 2004 kwa Kampuni ya Dhow Mercantile Limited. Ubinafsishaji huo uliipa kampuni hiyo 70% ya hisa na 30% ya hisa kubaki kwa Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Chai (MUVYULU). Baada ya ubinafsishaji, kulizuka mgogoro kati ya pande hizo mbili; hivyo, uendeshaji wa kiwanda na umiliki wa kiwanda uliosababisha DML kufungua kesi mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadaye pande hizo mbili zilikubaliana ya kumaliza mgogoro huo nje ya Mahakama chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina; ambapo kikao cha mwisho kilifanyika tarehe 13 Machi, 2026. Maazimio ya kikao hicho yanaendelea kufanyiwa kazi, ambapo ikikamilika, zoezi la kurejesha kiwanda litafanyika.