Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Eng. Johnston Johansen Mutasingwa (1 total)

MHE. ENG. JOHNSTON J. MUTASINGWA aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha upanuzi wa Kituo cha umeme Kibeta?
NAIBU WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Eng. Johnston Johansen Mutasingwa, Mbunge wa Bukoba Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa Serikali kupitia TANESCO inaendelea na upanuzi wa Kituo cha Kupooza Umeme cha Kibeta kwa kuongeza uwezo wa transfoma iliyokuwepo kutoka MVA 20 na kufunga transfoma yenye uwezo wa miundombinu ya Gridi ya Taifa ambapo utekelezaji wake umefikia 95% na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2026. Ahsante sana.