Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Dotto Jasson Bahemu (1 total)

MHE. DOTTO J. BAHEMU aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Nyakahura – Rulenge – Murugarama kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Nyakahura – Rulenge – Murugarama yenye urefu wa kilometa 85.6 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa sasa maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kuanzia Keza yanaendelea, ambapo tayari mkandarasi amepatikana na taratibu za malipo ya awali zinaendelea ili aweze kuanza kazi. Mara baada ya taratibu za malipo ya awali kukamilika kazi za ujenzi zitaanza. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuijenga barabara yote. (Makofi)