Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon William Kafiti Kafiti (3 total)

MHE. KAFITI W. KAFITI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa barabara ya Airport – Kayenze kilometa 34?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Kafiti William Kafiti Mbunge wa Ilemela kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa barabara ya Airport – Kayenze – Nyanguge yenye urefu wa kilometa 46 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Awamu ya kwanza inahusisha ujenzi kwa kiwango cha lami kuanzia maeneo ya Airport hadi Kibangaja (kilometa 10) ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia sita. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi.
MHE. KAFITI W. KAFITI aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha Kanuni za Bima za Kilimo ili kuongeza na kupatikana kwa kinga kwa wakulima na mazao mbalimbali?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa Fedha, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kafiti William Kafiti, Mbunge wa Jimbo la Ilemela, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na utafiti kuhusu bima katika mnyororo wa kilimo yaani mazao, mifugo, misitu na uvuvi ili kwa pamoja na mambo mengine kuwa na kanuni zinazovutia uwekezaji katika bima ya kilimo na kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima ili kupata huduma za bima kwa urahisi na haraka. Ni mpango wa Serikali kukamilisha uandaaji wa kanuni hizi katika kipindi cha mwaka 2026/2027. Naomba kuwasilisha.