MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji ulioko katika Kata ya Rwazera ni mradi ambao ni tegemezi kwa Kata ya Kamwanga, Bugalama, Isulwabutundwe, lakini ujenzi wa mradi huu unasuasua sana, je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kwenda nami kuuona huo mradi ili wasukume pesa ukamilike?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kasheku Musukuma kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa Mheshimiwa Kasheku Musukuma ameendelea kuwasiliana na Wizara ya Maji na ameendelea kuwasiliana na Mheshimiwa Waziri kuhakikisha kwamba tunachukua hatua katika mradi huu. Sasa kwa ombi lake hili mahsusi kwa Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri niko tayari kuongozana na Mheshimiwa Musukuma kwenda katika jimbo lake na kuangalia.