Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Edward Olelekaita Kisau (1 total)

MHE. EDWARD O. KISAU aliuliza: -

Je, lini mnara wa Redio Tanzania uliojengwa Kiteto utaanza kufanya kazi?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo hiki ni sehemu ya mradi unaotekelezwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). Hadi kufikia tarehe 14 Aprili, 2026 ujenzi na ufungaji wa miundombinu ya mitambo ya redio katika kituo hiki umefikia 90% na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2026. Ninakushukuru.