Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu 2026/2027–2050/2051, Mapendekezo ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2026/2027–2030/2031 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2026/2027; na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali Katika Muda wa Kati ya 2026/2027 hadi 2028/2029.
MHE. NABIL AHMED ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia hoja ya Dira ya Maendeleo, kweye Wizara ya Fedha. Wizara ya Kilimo imewekeza fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali ikiwemo umwagiliaji, vifaa vya kupimia udongo, matrekta na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukasema ili tuanzishe viwanda lazima tuzalishe malighafi ili viwanda hivi viweze kujiendesha na mdau mkubwa ni sekta binafsi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hili la sekta binafsi kuna mambo matatu:-
(i) Exchange rate;
(ii) World market price for commodity (kahawa, pamba, etc); na
(iii) Service levy.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunaanza msimu na rate ya shilingi 2,700 kwa USD moja, rate ya dola haipo stable, inakuja kushuka hadi shilingi 2,480 kwa dola na hapo alishasaini mkopo wa USD milioni 10; hapa amepata hasara ya exchange rate. Anakuja kupata hasara nyingine kwenye soko la dunia ikiwa bei ya zao kushuka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu, linapokuja suala la service levy, halmashauri zetu zinakusanya kodi hizi kwa turn over. Turn over hii inaingiza mkopo kutoka benki na riba zake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nishauri Wizara ya Fedha iangalie namna ya kuangalia ili service levy iweze kuwa-charged (kukusanywa) kutoka kwenye faida ya kampuni na sio turn over.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.