Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Amina Mussa Mkumba (1 total)

MHE. AMINA M. MKUMBA aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA katika Jimbo la Kibiti?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Amina Mussa Mkumba, Mbunge wa Kibiti, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Kibiti ni miongoni mwa ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi 65 vinavyoendelea kujengwa katika wilaya 64 na Mkoa mmoja wa Songwe. Ujenzi huo unafanyika katika wilaya au mkoa ambao hauna Chuo cha VETA.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Kibiti ambacho kinatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2026. Hadi sasa Serikali imeshatumia jumla ya shilingi bilioni 1.1 kati ya shilingi bilioni 1.6 zilizotengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza. Mpaka sasa ujenzi huo umefikia 69% ya utekelezaji wake.