MHE. TIMIDA M. FYANDOMO aliuliza: -
Je, hatua gani zimechukuliwa kulinda biashara na mitaji ya vijana dhidi ya ucheleweshaji wa malipo ya madeni ya wakandarasi?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na mimi kwa niaba ya Wazir wa FEdha ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Timida Mpoki Fyandomo, Mbunge wa Viti maalum.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitekeleza hatua mbalimbali za kuongeza na kulinda ushiriki wa vijana katika biashara. Kupitia Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali katika MUDA WA KATI (2026/2027 – 2027/2028), Maafisa Masuuli wa mafungu ya Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wameelekezwa kuzingatia mkakati wa kulinda wawekezaji wa ndani (local content) kwa kutoa kipaumbele cha kwanza katika zabuni, masharti ya mikataba na malipo ya hati za madai pamoja na kuweka msukumo katika joint venture kwa mikataba ya kigeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika kuhakikisha kuwa wakandarasi na wazabuni wanalipwa, mwaka 2025/2026 Serikali imetenga bajeti ya shilingi bilioni 700. Kwa kipindi cha Julai hadi Februari, 2026 kiasi cha shingi bilioni 477.6 kimelipwa. Aidha, Serikali itaendelea kulipa madeni ya wakandarasi ili kulinda mitaji yao pamoja na kuwezesha kuendelea kushiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo hapa nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.