Je, kuna mpango gani kufikisha huduma ya Maji Safi na Salama kutoka Ziwa Victoria kwa Wananchi wanaoishi umbali zaidi ya Km 12 kutoka Bomba Kuu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Tinnar Andrew Chenge, Mbunge Viti Maalum kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Mkoa wa Simiyu ambapo utekelezaji wa mradi huo utahusisha pia Vijiji 103 ambavyo viko katika umbali wa kilometa 12 kutoka bomba kuu kila upande katika Wilaya za Busega, Bariadi na Itilima. Mradi huo umefikia wastani wa 58% za utekelezaji ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2027.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali ni kuendelea kufanya upanuzi wa mradi huo mara utakapokamilika ili kufikisha huduma kwenye vijiji vyote ambavyo vitakuwa havijafikiwa na huduma ya majisafi na salama kadri fedha zitakavyokuwa zinapatikana.