Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Cosmas Mtesigwa Bulala (1 total)

MHE. COSMAS M. BULALA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao katika Kijiji cha Hungumalwa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuimarisha miundombinu ya uhifadhi wa chakula nchini, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali ilikamilisha ujenzi wa ghala 28 katika Mkoa wa Ruvuma yenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 28,000. Lengo ni kuhakikisha upotevu wa mazao ili kuimarisha usalama wa chakula nchini unapungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa na utaratibu wa kufanya tathmini kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa ghala katika Wilaya mbalimbali ili kubaini mahitaji halisi ya ghala. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, Wizara itafanya tathmini katika Wilaya ya Kwimba ili kubaini mahitaji halisi ya ghala kwa kuzingatia hali ya uzalishaji na mahitaji katika maeneo husika na itafanya maamuzi stahiki juu ya suala hili.