Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Asha Juma Feruz (4 total)

MHE. ASHA J. FERUZ: Mheshimiwa Mwenyekiti, jina langu ni
Asha Juma Feruz, Mwakilishi ninayewakilisha kundi la Vyuo Vikuu.
Ninaomba kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina mkakati gani
maalumu katika kutumia fursa za ajira katika kundi la vyuo na
vyuo vikuu kupitia mahusiano ya kikanda na kidiplomasia
tuliyonayo hasa zile kozi tunazoziita rare professionals? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA
MAHUSIANO (MHE. RAHMA R. KISUO): Mheshimiwa Mwenyekiti,
Serikali kwa kushirikiana na vyuo na vyuo vikuu, imeanzisha
mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo
katika ngazi mbalimbali za elimu za vyuo na vyuo vikuu na vyuo
vya kati ikiwa ni sehemu ya mtaala ili kuwawezesha kuhitimu elimu
katika ngazi hizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Serikali inatoa Mafunzo ya
Internship yanayojumuisha wahitimu wa ujuzi wa ngazi mbalimbali
za elimu hususan elimu ya juu na kati ambapo wanapatiwa fursa
ya kujifunza kwa vitendo mahali pa kazi. Lengo la mafunzo hayo
ni kuwapatia wahitimu ujuzi, maadili ya kazi, uzoefu na kufanya
kazi za taaluma zao na kuwawezesha kuajirika. (Makofi)
MHE. ASHA J. FERUZ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Waziri pamoja na ufafanuzi ulioutoa uchumi wa watu wa Kinondoni ambalo lipo Daraja la Tanzanite ni mkubwa kuliko uchumi wa watu wa Kigamboni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tozo inayotozwa pale kwenye Daraja la Kigamboni inasababisha nauli kuwa kubwa na kuendelea kuwafanya wananchi wa Kigamboni kuona kupita darajani ni kama adhabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuingia Kigamboni ni pesa na kutoka Kigamboni ni pesa. Ni lini mkataba huo ambao umeingiwa na Serikali pamoja na NSSF utakwisha kwa maana ya kulipa hilo deni na wananchi wa Kigamboni wanufaike na wao waone ni sehemu ya Tanzania na ku-enjoy kupita kwenye daraja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge, lakini niseme tu kwa swali la msingi lilivyokuja ningemuomba Mheshimiwa Mbunge muuliza swali atuletee swali la msingi tuliweze kulifanyia kazi ili tuweze kutoa maelezo yanayojitosheleza, ahsante.
MHE. ASHA J. FERUZ: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipatia nafasi niulize swali la nyongeza. Je Serikali ina mkakati gani mahususi wa kuchukua hatua kwa wawekezaji ambao hawarudishi hii CSR katika maeneo yetu? Maana wapo wawekezaji ambao hawarudishi kabisa na wameshawekeza kwa muda mrefu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Asha Feruz, kwa kuwatetea wananchi ambapo wawekezaji wetu wameweka miundombinu au uwekezaji kule wa kupitia CSR (Corporate Social Responsibility). Ni kweli tunapokea changamoto kutoka kwa baadhi ya wawekezaji ambao hawa-comply na ile sheria yetu ya local content na tumekuwa tukishirikiana na Wizara za Kisekta, kwa sababu hii miradi ipo kwenye sekta mbalimbali; kwa watu wa ujenzi, kuna miradi kama hii, watu wa uchukuzi, watu wa kilimo na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi kama Serikali tupo on top of that na tutahakikisha tunashirikiana na Wizara nyingine ku-address haya matatizo tuhakikishe ile CSR sasa inalipwa kulingana na sheria ambayo imetungwa, ninashukuru.
MHE. ASHA J. FERUZ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kwanza ninampongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuri anayoifanya. Kutokana na majibu ya swali la msingi, kwamba ni kweli vipo vyuo ambavyo vinatoa kozi ambazo hazipo kwenye kada za Sekretarieti, je, ni upi mkakati wa Serikali sasa kuweza kuwa-accommodate kwa haraka wale wanafunzi ambao tayari wameshamaliza masomo kwenye hizo kozi ambazo hazipo kwenye kada za Sekretarieti, kwa sababu tayari zilisharuhusiwa kufundishwa kutokea Serikalini, zilipewa kibali?
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza na mimi nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Pia, niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa pole kwa familia ya Mheshimiwa Saashisha Mafuwe kwa msiba mkubwa wa mama yake, Mwenyezi Mungu amhifadhi na aendelee kuwapa faraja familia nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali la nyongeza lililoulizwa na Mheshimiwa Mbunge, ukweli ni kwamba Serikali imekuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na vyuo vikuu pale wanapounda kozi au eneo lolote la masomo. Ninataka nitoe mfano ili jibu liwe jepesi. Chuo Kikuu Mzumbe wana kozi inaitwa Maendeleo ya Vijana. Kozi ile inatengeneza maafisa vijana. Kama unavyojua, kwenye Serikali mfumo wetu sisi unazo nafasi kwenye TAMISEMI za maafisa wa vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ile kozi walikuwa hawajaingizwa katika muundo. Tunapozungumza sasa hivi, Serikali imeshakamilisha mawasiliano kwanza ndani ya Serikali, na pia kutengeneza muundo ambao vijana wale ambao wamemaliza kozi ile wote wanakwenda kuwa adopted katika mfumo wa ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunachokifanya ambacho ameeleza Mheshimiwa Naibu Waziri, ninataka nieleze, ni yaleyale, kwamba msingi mkubwa, vyuo vikuu viwasiliane na Wizara husika kwa maana ya Wizara mama kama Wizara ya Elimu ili sisi ambao tunahusika na kutengeneza miundo ya kazi, tuweze kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha kwamba watu wote wanaomaliza vyuo vikuu tunawa-adopt katika mfumo wa kazi, waingie katika mfumo wa ajira ili waweze kupata kazi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninashukuru.