Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Dr. George Venance Lugomela (1 total)

MHE. DKT. GEORGE V. LUGOMELA aliuliza:-
Je, lini Barabara kutoka Senani hadi Gula itakarabatiwa ili iweze kupitika wakati wa masika?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. George Venance Lugomela, Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Senani – Gula ni barabara inayounganisha Kata ya Senani, Mpindo na Kata ya Lalago katika Barabara ya Senani – Zebeya – Lalago katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa yenye urefu wa kilometa 38.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imeanza kufanya ukarabati wa barabara hiyo urefu wa kilometa 12 kwa gharama ya shilingi milioni 125, ambapo kazi hiyo inaendelea na mkandarasi anaendelea na kazi. Kazi nyingine zinazoendelea katika barabara hiyo ni pamoja na kunyanyua tuta meta 320, kujenga makalavati mistari mitatu na kuchimba mitaro kilometa 6.6.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuendelea na ukarabati wa barabara hii, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali imetenga shilingi milioni 200 kwa utekelezaji. Ahsante.