Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 636 2025-06-20

Name

Nicholaus George Ngassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuunganisha kipande cha Mbutu na Igunga Mjini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kipande cha barabara ya Mbutu hadi Igunga Mjini chenye urefu wa kilometa tano na imepanga kufanya usanifu wa kina katika mwaka wa fedha 2025/2026. Hatua hii inalenga kubaini gharama halisi za ujenzi, mahitaji ya kiufundi na kuandaa nyaraka za zabuni zitakazotumika wakati wa utekelezaji wa mradi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kukamilika kwa usanifu huo, Serikali imepanga kuanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami kuanzia mwaka wa fedha 2026/2027 kulingana na upatikanaji wa fedha.