Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 5 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 72 2026-02-02

Name

Paschal Inyasi Chinyele

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Primary Question

MHE. PASCHAL I. CHINYELE aliuliza:-

Je, kwa nini wananchi wa Kata ya Mbalawala wamezuiwa kuendeleza ardhi wanayomiliki kwa maelezo kuwa ni sehemu ya Bonde la Kati Singida?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Paschal Inyasi Chinyele, Mbunge wa Dodoma Mjini. Bonde la Mzakwe linasimamiwa na Mamlaka ya Bonde la Wami Ruvu Water Basin na Mamlaka ya DUWASA na siyo Bonde la Kati la Singida kama swali lilivyoelekezwa. Bonde hili lilipimwa kisheria na kusajiliwa Aprili, 2000 kwa ramani yenye Namba 45977.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hilo lina ukubwa wa hekta zaidi ya 34,000 na lipo katika Kata za Chihikwi, Kawawa, Matangizi, Makulu na Mtaa wa Muungano.

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu zilizopelekea kuzuiwa kufanya maendelezo katika bonde hilo ni kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kuwa kuna zaidi ya visima 20 vinavyotoa huduma ya maji yanayotumika na wananchi wa Dodoma Mjini na maeneo jirani, eneo ilo kitaalam lina kimo cha maji kilichopo juu. Serikali imechukua hatua za kusitisha upimaji na umilikishaji pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari ya kuendeleza eneo hilo.