Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 14 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 164 2026-04-22

Name

Dr. Regina Christopher Malima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. REGINA C. MALIMA aliuliza:-

Je, Serikali imejipangaje kuboresha Programu za Uanagenzi, Ufundi Stadi na Ubunifu ili kuwawezesha Vijana kujiajiri na kuondoa changamoto ya ajira?

Name

Wanu Hafidh Ameir

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Dkt. Regina Christopher Malima kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeendelea kueneza Mpango wa Mafunzo kwa Mfumo wa Uanagenzi Pacha (Dual Apprenticeship Training System) ambapo mafunzo yanatolewa kwa kushirikiana na viwanda. Mfumo huu unaendeshwa kwa utaratibu Ungwe (Block Release) ambapo wanafunzi hujifunza kwa kubadilishana muda wa kuwa chuoni kisha viwandani na sehemu za kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo huu unawawezesha wanafunzi kupata umahiri kwa haraka na fursa za ajira pindi wanapohitimu. Kwa sasa mfumo wa DATS unatumika kwa fani za kilimo, ukarimu, utalii, ufundi magari, ufundi umeme na programu za madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeandaa mikakati ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano na viwanda na waajiri; kujenga uelewa kwa wadau wa viwanda (Industrial Mentors) na kueneza mfumo wa DATS kwa kuongeza fani za mafunzo na Vyuo.