Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 46 2026-04-10

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za watumishi wa afya ngazi ya kata katika Jimbo la Nanyumbu?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Ally Mhata, Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI.
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na nyumba za watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Kutokana na ongezeko la ujenzi wa vituo vipya, kumepelekea mahitaji makubwa ya nyumba za watumishi.

Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya tathmini ya mahitaji ya nyumba za watumishi ambapo jumla ya nyumba 25,690 zinahitajika kote nchini, nyumba za watumishi zilizopo ni takribani 7,696 sawa na 30%. Aidha, katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu takwimu zinaonesha kunahitajika nyumba 147 na zilizopo ni 43 sawa na 29%.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu imetenga jumla ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za watumishi kwenye Kituo cha Afya Mnanje na Zahanati ya Kazamoyo.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.