Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kata ya Nsalala Wilayani Shinyanga?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, nashukuru sana kwa majibu ya Naibu Waziri na kwa kazi ambayo Serikali imeanza kuifanya katika Kata ya Nsalala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Shinyanga, kata zote 26, ni Kata ya Nsalala peke yake ndiyo ambayo haina hata zahanati. Kwa hiyo, kwa utaratibu huu ambao Serikali imeuanzisha, nawapongeza sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza. Kwa kuwa, Shinyanga DC ina maboma zaidi ya 56 ambayo yako katika level tofauti, nini mpango mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba yale maboma ambayo wananchi walijitolea nguvu na fedha zao kwa ajili ya kuyaanzisha yanakamilika?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa, hata Halmashauri ya Shinyanga, majengo ya hospitali ya wilaya hayajakamilika, ni upi Mpango wa Serikali?
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tupokee pongezi ambazo Mheshimiwa Mbunge Christina Christopher Mnzava amezitoa. Serikali inatambua idadi ya maboma iliyonayo katika utekelezaji wa kuyakamilisha. Tuna maboma ya vituo vya afya 341, lakini tuna maboma ya zahanati 1,841.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejipanga, kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma haya na tayari tumeanza kuyatengea bajeti pia. Kupitia fedha za ndani, tumewaelekeza Wakurugenzi wetu kutenga fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma hayo, lakini pia, fedha kutoka Serikali Kuu nazo zitakwenda kusaidia kukamilisha maboma
Name
Esther Lukago Midimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kata ya Nsalala Wilayani Shinyanga?
Supplementary Question 2
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Buchambi, Wilaya ya Maswa ina wakazi wengi, lakini haina kituo cha afya. Je, ni lini Serikali itajenga kituo cha afya kwa Kata ya Buchambi? (Makofi)
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa katika Bunge lako Tukufu tayari tulishapeleka fedha za kujenga vituo vya kimkakati katika Majimbo 120. Majimbo mengine 94 tumeshayaombea fedha Hazina, nayo yatapata kwa awamu ili kuweza kukamilisha ujenzi wa vituo hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge Esther kwamba Wilaya ya Maswa ni wanufaika katika ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati. (Makofi)
Name
Nuru Issa Kashakari
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Kusini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kata ya Nsalala Wilayani Shinyanga?
Supplementary Question 3
MHE. NURU I. KASHAKARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninaomba kuuliza swali la nyongeza kwa Mheshimiwa Naibu Waziri. Je, ni lini Serikali itakamilisha Kituo cha Afya cha Kazulamimba, Kituo cha Afya cha Kata ya Mwakinzega na ni lini pia Serikali…
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge swali la nyongeza ni moja tu.
MHE. NURU I. KASHAKARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge akiulizia kuhusu Kituo cha Afya cha Kazulamimba. Kituo cha Afya cha Kazulamimba ni pamoja na vituo vya afya 341 ambavyo tumeviainisha. Tutaendelea kutenga fedha za ndani za halmashauri na zile za Serikali Kuu ili kuhakikisha kituo hiki cha afya kinaanza kutoa huduma kwa wananchi wetu. (Makofi)
Name
Kiza Hussein Mayeye
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kata ya Nsalala Wilayani Shinyanga?
Supplementary Question 4
MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Afya inataka kila Kata kuwa na kituo cha afya, lakini katika Jimbo la Kigoma Kaskazini mpaka sasa Kata za Mkongoro, Mkigo, Nyarubanda, Nkungwe, Mungonya, Kidahwe na Matendo hawana vituo vya afya na wakinamama wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma ya afya. Ni lini Serikali itakamilisha sera hii kwa kuleta vituo vya afya katika Kata hizi? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Kiza Mayeye, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, kwa kazi kubwa anayoifanya hapa Bungeni ya kufuatilia maendeleo ya Jimbo la Kigoma Kaskazini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali ni kujenga vituo vya afya katika Kata zote. Awali tulianza na zile Kata za kimkakati kulingana na mahitaji na vipaumbele. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Kiza Mayeye, ndani ya awamu hii tunakwenda kujenga vituo vya afya kulingana na vipaumbele katika Jimbo la Kigoma Kaskazini. (Makofi)
Name
Christina Solomon Mndeme
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kata ya Nsalala Wilayani Shinyanga?
Supplementary Question 5
MHE. CHRISTINA S. MNDEME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii na mimi niulize swali la nyongeza. Katika Zahanati ya Imalakaseko iliyopo Kata ya Goweko, Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora, Serikali ilitoa shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na mtoto lakini wodi hiyo bado haijakamilika. Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha ujenzi wa wodi hiyo ya mama na mtoto katika zahanati ya Imalakaseko, Kata ya Goweko, Halmashauri ya Wilaya ya Uyui? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge amegusia hasa katika zahanati ya Imalakaseko, Halmashauri ya Uyui. Kwanza Serikali imeshatenga shilingi milioni 80 kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema. Pia, ninamwelekeza Mkurugenzi kuendelea kutenga fedha za ndani Halmashauri ya Uyui ili kuweza kukamilisha ujenzi wa zahanati hii. (Makofi)
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kata ya Nsalala Wilayani Shinyanga?
Supplementary Question 6
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya Lukozi ni kati ya vituo vya kimkakati ambavyo vimetengewa fedha na Serikali. Ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa kituo hicho?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tunaipongeza Serikali kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari kilipelekewa fedha shilingi milioni 250 za awali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunaombea wale Waheshimiwa Wabunge ambao hawajapata, yale Majimbo 94, lakini tumeshawaelekeza Wakurugenzi wote katika Halmashauri kuendelea kutenga fedha za ndani ili kuhakikisha huduma zinatoka katika vituo vyetu vya afya, na maeneo yote yenye upungufu tutayaombea fedha Hazina. (Makofi)