Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. TIMOTH G. ANYOSISYE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga kingo za zege za Mto Mbezi ili kuzuia kusombwa kwa nyumba na kusababisha maafa?
Supplementary Question 1
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, hivi karibuni katika Mto Kikafu, lile daraja, kumekuwa kukitokea ajali nyingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa Barabara ya Moshi – Arusha, lakini barabara pekee ambayo ni ya mchepuko na ya mbadala ni Bomang’ombe - Chekimaji TPC, ambayo inajengwa kilometa 3.5. Je, ni lini sasa Serikali italeta fedha ya kumaliza barabara hii ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami na taa juu? Ahsante.
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa Barabara ya Bomang’ombe - Chekimaji TPC. Kama ambavyo imeanishwa kwenye mipango yetu, Serikali itatenga fedha, kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii, kilometa 3.5, kwa kiwango cha lami mara tu baada ya fedha hizi kupatikana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved