Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Edibily Kinyoma Kazala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kasulu Vijijini

Primary Question

MHE. EDIBILY K. KINYOMA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwalipa fidia Wananchi wa Kitongoji cha Katoto waliopisha Mradi wa Kitalu cha Makere Forest Reserve?

Supplementary Question 1

MHE. EDIBILY K. KINYOMA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Serikali, bado nina swali moja la nyongeza la kuiomba Serikali kama Mheshimiwa Waziri yuko tayari tuambatane naye kuelekea jimboni akaone na kujidhirisha namna zoezi lilivyotekelezwa na kusaidia kutatua migogoro inayoambatana na kitalu hiki cha Makere Forest Reserve Uvinza Open Area.

Mheshimiwa Spika, kitalu ambacho kinasabaisha mgogoro wa wananchi; wananchi kufyekewa mazao, kupigwa na kuna mgogoro wa kimapato na halmashauri kwa mfano kwa DCC ripoti tuliopata wanapata kama 1,900,000 tu. Pia kuna mgogoro wa Kacheri na Luguvu Relini ambao nao wameambiwa kuhamishwa, kuna mgogoro wa wananchi wenyeji nao wamechukuliwa maeneo yao na wakati walikuwepo pale tangu miaka ya 70.

Mheshimiwa Spika, pia kuna mgogoro wa TFS na wananchi wa kimpaka, wananchi wamewekewa beacon mpaka katikati ya vijiji. Ninaomba ikiwezekana Mheshimiwa Waziri aambatane nami twende jimboni kupunguza changamoto zinazokabili jimbo langu. Ahsante sana.

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mimi niko tayari hata tukimaliza Bunge twende kwa wananchi wetu kuweka tabasamu kuondoa migogoro ambayo inawakabili. (Makofi)