Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Suleiman Mohamed Rashid

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwera

Primary Question

MHE. SULEIMAN MOHAMED RASHID aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha maslahi na stahiki za Walimu wanaosahihisha Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne na Sita?

Supplementary Question 1

MHE. SULEIMAN MOHAMED RASHID: Mheshimiwa Spika, ahsante nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri lakini pamoja na majibu hayo nina swali la nyongeza. Serikali haioni haja kuandaa mwongozo wa dharura wa uboreshaji ambao utaweza kuzingatia kulipwa kwa posho ya kujikimu pamoja na posho maalum kwa walimu ambao wanasahihisha mitihani hiyo?

Name

Omari Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako, ninaomba nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikiboresha maslahi ya walimu wanaosahihisha mitihani kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo pamoja na posho wanazolipwa Serikali pia hulipa malazi, chakula, matibabu wakati wote wa kazi. Hata hivyo, ushauri wa Mheshimiwa Mbunge tumeupokea. (Makofi)