Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, kwa nini, Serikali isianzishe eneo mahsusi la viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya misitu litakalohudumia masoko mbalimbali?

Supplementary Question 1

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa majibu yaliyotolewa na Serikali kutambua umuhimu wa jambo hilo, lakini nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutenga maeneo ni jambo moja na kuhakikisha kwamba maeneo hayo yanapata hivyo viwanda ni jambo la pili. Sasa Serikali haioni umuhimu, kwa sababu maeneo mengi yaliyotengwa wanajenga viwanda Dar es Salaam, Pwani na maeneo ya mijini. Serikali haioni umuhimu wa kutenga vivutio mahususi kwenye maeneo ya vijijini ambako kule ndiko kwenye ajira kubwa, katika muktadha wa business as usual ambayo Wizara hii ndiyo imejirasimu nao? (Makofi)

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini, kwanza kwa kuwatetea wananchi wa Njombe Mjini. Mheshimiwa Mwanyika, amekuwa akifuatilia sana suala la uwekezaji kwenye mazao ya misitu nasi kama Wizara tunamuahidi kumpa ushirikiano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba huko nyuma viwanda vingi vili-concentrate upande wa Pwani, Mikoa ya Pwani Dar es Salaam na Tanga, ndiyo maana katika mpango wa miaka mitano wa Serikali tumekuja na mkakati wa ku-decentralize viwanda vyetu kupeleka kila maeneo. Kwa kupitia hilo tumeanzisha mpango wa maeneo maalum ya uwekezaji na ndiyo maana upande wa Njombe tunaenda kuanzisha maeneo maalum ya uwekezaji wa misitu, upande wa Bunda tunaenda kuanzisha Bunda SEZ ambapo tunaenda kuanzisha maeneo maalum kwa ajili ya mazao ya blue economy, vilevile Kigoma upande wa michikichi na mihogo na hapa Dodoma tuna eneo maalum kwa ajili uchenjuaji wa madini ambayo ni adimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kupitia hii nina uhakika sasa, ile adha kwamba viwanda vyote vime-concentrate ukanda moja inaenda kwisha na ninaomba nimtoe mashaka Mbunge kwamba tunaenda kutekeleza hili katika Mkoa wa Njombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana. (Makofi)

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, kwa nini, Serikali isianzishe eneo mahsusi la viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya misitu litakalohudumia masoko mbalimbali?

Supplementary Question 2

MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nami nafasi ya swali la nyongeza. Serikali ilitoa maelekezo kwa Halmashauri zote kutenga maeneo ya kongani za viwanda. Sasa ni upi mpango wa Serikali kufanya uwekezaji katika maeneo ambayo yamekwishatengwa hasa ya usindikaji wa mazao ya kilimo? (Makofi)

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la moja la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kutoka Mkoa wa Manyara kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Rais na tunakumbuka wakati anazindua Bunge letu alitoa maelekezo kwa Wizara yetu tuhakikishe kwamba tunaanzisha kongani za viwanda kila wilaya. Katika bajeti ya mwaka huu ambayo ilipitishwa wiki iliyopita, tayari tumeweka mipango ya kuhakikisha kwamba tunaenda kuanzisha kongani za viwanda kila wilaya. Lengo ni kuhakikisha kwamba tunasogeza huduma za uwekezaji karibu na wananchi hususani katika kusaidia wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatambua Mkoa wa Manyara ni mojawapo ya maeneo ambayo kimsingi ni potential kwa ajili ya kilimo cha ngano na tayari tunayo kongani ya viwanda kubwa kule, ninaomba nimuahidi Mbunge kwamba vilevile Mkoa wa Manyara upo ndani ya mipango yetu ya kuanzisha kongani za viwanda na tutaviendeleza. (Makofi)