Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephine Joseph Kapoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA K.n.y. MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza Miradi ya TACTIC iliyopangwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, wafanyabiashara hawa waliahidiwa soko hili kuanza tangu Julai, 2025 na mpaka sasa wanashindwa kufanya biashara zao kwa sababu hawajui hatima yao. Je, ni lini sasa Serikali inategemea kuanza mradi huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, tuna miradi kadhaa Mkoa wa Morogoro ambayo inatakiwa, iko chini ya TACTIC. Je, ni lini Serikali inajipanga kuanza kukamilisha kwa sababu mingi iliahidiwa tangu mwaka 2025?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali inatekeleza miradi hii ya TACTIC; tunayo makundi matatu. Kuna kundi la kwanza la miji 12, kundi la pili la miji 15 na kundi la tatu ambalo Ifakara imo ni miji 18.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tayari imeshaanza utekelezaji wa miradi hii katika makundi ya kwanza na ya pili na utekelezaji unaendelea. Ipo miradi iliyokamilika, ipo ambayo inaendelea na hatua mbalimbali. Baada ya kukamilisha usanifu wa miradi hii ya kundi la tatu, tutaanza utekelezaji wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Kilombero na Ifakara kwamba Serikali baada ya kukamilisha usanifu wake tutaanza mara moja utekelezaji wa mradi katika eneo la Ifakara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, tunafahamu kuwa iko miji kadhaa ambayo iko kundi la tatu, la kwanza na la pili ambayo inaendelea na utekelezaji wa miradi ya TACTIC. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama ambavyo utekelezaji unaendelea, tutahakikisha inakamilika kwa wakati. Ile ambayo haijaanza, na ambayo iko tier three tutahakikisha nayo inaanza kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inatekelezwa kwa wakati.

Name

Sara Msafiri Ally

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA K.n.y. MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza Miradi ya TACTIC iliyopangwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara?

Supplementary Question 2

MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Jimbo la Mvomero kwenye Tarafa ya Turiani ambayo ni ya kimkakai ya kiuchumi haina miundombinu ya barabara wala masoko. Je, Serikali haioni kwamba ipo haja ya kuiweka miradi hii kwenye mpango wa miradi ya TACTIC ili kuongeza uchumi wa wananchi wa Turiani?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kweli kwamba Jimbo la Mvomero Tarafa ya Turiani ni moja ya maeneo ambayo yanakua kwa kasi kwa kuwa na shughuli nyingi za kiuchumi na za kijamii na zinahitajika barabara, masoko, stendi na miundombinu mingine ya kiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Sara Msafiri kwamba, kwa sasa mradi wa TACTIC unatekelezwa kwenye miradi ambayo ilishafanyiwa design kwenye miji 45. Kwa hiyo, tutaendelea kutenga fedha kwa ajili ya maeneo ambayo hayapo kwenye miradi ya TACTIC, ikiwemo Mvomero, kuhakikisha tunajenga barabara hizo kwa awamu, lakini pia kuhakikisha kwamba tunajenga miundombinu kama masoko ili wananchi wa Turiani na Mvomero kwa ujumla wapate huduma bora.

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA K.n.y. MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza Miradi ya TACTIC iliyopangwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara?

Supplementary Question 3

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Halmashauri ya Mji wa Nanyamba inatekeleza mradi wa TACTIC kwenye awamu ya tatu. Timu mbalimbali za TAMISEMI zikifika, kumekuwa na kubadilikabadilika kwa miradi itakayotekelezwa phase one.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna timu ilituambia tutaanza mradi wa kituo cha mabasi na barabara kilomita tano na kuna timu wanatuambia kuna barabara kilomita tano, stendi na soko. Je, Serikali itatamka rasmi sasa kwamba awamu ya kwanza Nanyamba tutafanya kitu gani?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge wa Nanyamba, Mheshimiwa Chikota, kwamba Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ipo katika mradi wa TACTIC awamu ya tatu. Hivi sasa kazi ya usanifu iko hatua za mwisho kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi ule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi ule una package tofauti. Ninaomba nitumie nafasi hii nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, baada ya session hii ya maswali na majibu nitafuatilia nimpe hakika na awamu ya kwanza ni mradi ipi na awamu ya pili ni mradi ipi ili kusiwe na kubadilikabadilika kwa miradi ambayo itatekelezwa.

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA K.n.y. MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza Miradi ya TACTIC iliyopangwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Songea Mjini ni mmoja kati ya maeneo ambayo miradi ya TACTIC inatekelezwa. Mradi wa ujenzi wa masoko ya Manzese A na B umechukua muda mrefu sana. Je, ni lini ujenzi huo utakamilika? Ahsante sana.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Ndumbaro, Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini kwamba Serikali inafahamu kwamba utekelezaji wa mradi wa TACTIC katika Manispaa ya Songea unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kuna baadhi ya miradi haijakamilika kwa wakati. Tumeshachukua hatua kwa kukaa na mkandarasi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba anaongeza kasi na kukamilisha ile miradi mapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI tunafuatilia kwa karibu, na tutahakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika ili iweze kuleta tija inayokusudiwa kwa wananchi wa Manispaa ya Songea.