Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dickson Nathan Lutevele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Primary Question
MHE. DICKSON N. KUTEVELE K.n.y. MHE. JESCA J. MAGUFULI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha vijana wanapata ujuzi sahihi na kunufaika kupitia Akili Mnemba (AI)?
Supplementary Question 1
MHE. DICKSON N. LUTEVELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Ninaomba nimwulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa teknolojia hii ya AI ndiyo inayoongoza dunia kwa sasa, na mara nyingi fursa kama hizi zinawapata tu vijana wa mjini, je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuhakikisha kwamba teknolojia hii mnazunguka hasa vijijini ikiwemo maeneo ya mikoani kama Mafinga kwa ajili ya kuwafundisha vijana wote ili waweze kupata fursa hii? (Makofi)
Name
Switbert Zacharia Mkama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuwafikia vijana katika maeneo ya mikoa mbalimbali, ndiyo sababu nimeeleza kwamba tumeanza utaratibu wa kujenga vitu vya ubunifu nchini. Tumeanzia na mikoa ambayo nimeitaja, Mikoa ya Lindi, Dodoma, Tanga, Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya, na Zanzibar, na tutaendelea hatua kwa hatua kuwekeza katika mikoa mingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, Serikali inashirikiana na wadau mbalimbali wa Kimataifa. Kwa mfano, tunashirikiana na International Telecommunication Union (ITU), wanafanya mradi na Tume ya TEHAMA. Huu mradi unaitwa ITU IA For Good Sandbox. Mradi huu unatekelezwa kwa vijana wote nchini bila kujali ni wa mjini au wa vijijini, kwa lengo la kuwapa uwezo wa kutengeneza mifumo ya AI.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali inalitambua hilo, na pia inashirikiana na UNESCO kuwekeza katika maeneo haya. Hili litahusisha watumishi wote wa Serikali walio mjini na maeneo yote ya nchini, vijijini na kila sehemu kwa kuwajengea uwezo wa eneo hili la akili mnemba.
Name
Mabula Johnson Magangila
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Msalala
Primary Question
MHE. DICKSON N. KUTEVELE K.n.y. MHE. JESCA J. MAGUFULI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha vijana wanapata ujuzi sahihi na kunufaika kupitia Akili Mnemba (AI)?
Supplementary Question 2
MHE. MABULA J. MAGANGILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa katika Sekta ya Elimu tumekuwa tukihangaika na walimu wengi kwa baadhi ya masomo kama Sayansi na Biashara, je, ni lini Serikali sasa itatumia teknolojia hii kutengeneza walimu ambao wataenda kufundisha masomo ambayo yana upungufu wa walimu watokanao na akili mnemba? (Makofi)
Name
Switbert Zacharia Mkama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu langu la msingi nimeeleza kwamba, Serikali kupitia Tume ya TEHAMA imepitia mitaala 111 ya vyuo vikuu 32 vyenye mlengo wa TEHAMA. Hivi vyuo vingine vinawafundisha walimu, kwa hiyo, hii mitaala ambayo tumeipitia itahakikisha kwamba tunatoa wataalamu wanaotumia akili mnemba wakiwemo walimu, ili waende kufundisha katika shule wanazozitumikia.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved