Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Charles Jacob Sungura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Kwedikwazu - Sindeni inayopitia Daraja la Komdudu ambayo ipo kwenye Mradi wa World Bank kwa kiwango cha Lami?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri. Kwa kuwa barabara ya Michungwani - Kwadoya yenye urefu wa kilometa 19 nayo ni sehemu ya utekelezaji wa barabara za awamu ya pili (second road generation) na zabuni barabara hii ishatangazwa, je, ni lini sasa Serikali itatoa barua ya tuzo (letter of award) ili ujenzi wa barabara hii nao uanze kwa kiwango cha lami?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lingine la pili. Kwa kuwa barabara ya Mkata kwa Sunga yenye kilometa 21 nayo ni miongoni mwa utekelezaji wa barabara za third generation road wa RISE, sasa ni lini Serikali itatangaza zabuni ili ujenzi wa barabara hii nao uanze kwa kiwango cha lami? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimthibitishie Mheshimiwa Sungura, Mbunge wa Handeni, kwamba Serikali inatambua muhimu wa barabara hizo na ndiyo maana tayari tumeanza na hii barabara, na tayari zabuni imeshasainiwa, mkataba ushasainiwa tayari kwa kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia tunafahamu na hizo barabara nyingine mbili, moja ambayo Mheshimiwa Mbunge angependa ifanyiwe matangazo na mzabuni apatikane. Nimhakikishie tu kwamba suala hilo tumelichukua, tutalifanyia kazi kwa barabara zote mbili ili tuweze kutangaza zabuni kwa kadri fedha zitakavyopatikana kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hizo.
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Kwedikwazu - Sindeni inayopitia Daraja la Komdudu ambayo ipo kwenye Mradi wa World Bank kwa kiwango cha Lami?
Supplementary Question 2
MHE. EXAUD S. KIGAHE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Jimbo la Mufindi Kaskazini tuna mradi huu wa Kata ya Ifwagi, Mdabulo na Ihalimba. Ni lini Serikali itaanza kukamilisha ujenzi wa kilometa 16 kutoka Kata ya Ifwagi mpaka Mdabulo na kilometa 10 kutoka Kata ya Ifwagi mpaka Ihalimba? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Kigahe, Mbunge wa Mufindi Kaskazini, alishawahi kuwasilisha barabara hiyo na tayari Serikali ilianza hatua za ujenzi kwa awamu wa barabara hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kutenga fedha kwenye bajeti kwa awamu kuhakikisha kwamba barabara hiyo inajengwa kwa awamu na kuhakikisha kwamba tunafikisha lengo la wananchi kupata usafiri mzuri katika Jimbo la Mufindi Kaskazini.
Name
Cornel Lucas Magembe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato Kaskazini
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Kwedikwazu - Sindeni inayopitia Daraja la Komdudu ambayo ipo kwenye Mradi wa World Bank kwa kiwango cha Lami?
Supplementary Question 3
MHE. CORNEL L. MAGEMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi ili kuuliza swali la nyongeza. Katika mji maarufu wa Chato kuna zaidi ya kilomita nne ambazo tayari Serikali ilikuwa ianze ujenzi wake mwaka 2025, lakini mpaka sasa haujaanza kutekelezwa. Pia iko barabara ndogo pale Mji wa Mganza zaidi ya kilomita moja na nusu ambao nao ujenzi wake haujaanza. Je, ni lini Serikali inakwenda kuanza ujenzi wa barabara hizo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa barabara hizi unafanyika kwa awamu na Serikali inaendelea kutenga fedha kwenye bajeti zake ili kila mwaka wa fedha tuendelee na hatua moja ya ujenzi ili kukamilisha ujenzi wa barabara hizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Chato Kaskazini kwamba Serikali itatekeleza azma yake na hadhi yake ya kujenga barabara hizo.
Name
Kija Limbu Ntemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Katoro
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Kwedikwazu - Sindeni inayopitia Daraja la Komdudu ambayo ipo kwenye Mradi wa World Bank kwa kiwango cha Lami?
Supplementary Question 4
MHE. KIJA L. NTEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuna barabara inayotoka Mererani kwenda Hospitali ya Wilaya ya Katoro imeharibika sana, siyo kwa sababu ya mvua tu, bali ni muda mrefu. Hata kama nilimwelezea Mheshimiwa Naibu Waziri, haitoshi. Je, yuko tayari baada ya Bunge hili tuambatane sote tukakague zile barabara na kuhimiza ili ziweze kujengwa kutoa huduma nzuri kuelekea katika hospitali ya Wilaya ya Katoro?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, niko tayari tuongozane na Mheshimiwa Ntemi kwenda Jimbo la Katoro ili tupitie barabara hiyo. Hata hivyo, ninaamini tayari ipo kwenye mipango yetu, tutakwenda kusukuma pia mipango hiyo ili barabara hiyo iweze kupata fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wake.
Name
George Natany Malima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Kwedikwazu - Sindeni inayopitia Daraja la Komdudu ambayo ipo kwenye Mradi wa World Bank kwa kiwango cha Lami?
Supplementary Question 5
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ni lini Serikali itajenga daraja linalounganisha Mji wa Mpwawa?
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa hujawasha kisemeo chako.
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ni lini Serikali itajenga daraja linalounganisha Mji wa Mpwawa na Kijiji cha Iyomo, kwa kuwa kwa sasa hakuna mawasiliano kufuatia mvua kubwa zilizonyesha na kuharibu miundombinu ya daraja hili?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba barabara zetu zinapitika vizuri na madaraja yanajengwa ili kurahisisha huduma za usafiri kwa wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nichukue hoja ya Mheshimiwa Malima, Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, na nichukue nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kumwelekeza Meneja wa TARURA wa Mpwapwa wawasilishe tathmini ya mahitaji ya fedha ya daraja hilo ili Serikali iendelee na mipango yake ya kutafuta fedha kwa ajili ya kwenda kujenga daraja hilo.