Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Neema Peter Majule
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. NEEMA P. MAJULE aliuliza: - Je, Serikali imeweka vivutio gani vya uwekezaji kwa Wazawa ili kuwahamasisha kuwekeza zaidi nchini?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. NEEMA P. MAJULE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, pia kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, kuhusu vivutio ambavyo Serikali imevi-identify kabisa kwa ajili ya wawekezaji hasa wazawa, lakini kuna sheria za TRA ambazo bado zinakinzana na hivyo vivutio, ikiwepo hiyo tax exemption katika import duty, bado kuna shida lakini pia hiyo tax holiday ambayo amesema kuna grace period, inabidi wasubiri, bado kuna shida. Wenyewe TRA, wanaongozwa tu na sheria zao. Niulize sasa, je, Serikali imejipangaje ku-harmonize vivutio vyake na sheria za TRA? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Wawekezaji wengi wageni wameingia hapa kwetu na hivyo wawekezaji wazawa wakiwepo wawekezaji wa kati na wadogo wanashindwa kuhimili ushindani wa uwekezaji wa nje. Je, Serikali imejipangaje kuwaandaa wawekezaji wetu wa ndani, wengi wao wakiwa ni wanawake na vijana, kuhimili ushindani wa kibiashara na wale wawekezaji wa nje? (Makofi)
Name
Dr. Pius Stephen Chaya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Neema Peter Majule, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma kwa maswali yake mawili ya nyongeza. Mara kwa mara amekuwa akichangia sana kwenye suala la uwekezaji na hususan kuwatetea wanawake wa Dodoma kwenye masuala ya uwekezaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, hivi vivutio vimepitishwa na wenzetu wa Wizara ya Fedha, na TRA wamehusika katika kuvipitisha, lakini ninatambua kuna changamoto za hapa na pale katika administration ya hii certificate of incentives ambayo kimsingi sisi kama Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, vilevile tumekuwa tukipokea hiyo changamoto kutoka kwa wawekezaji wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, tumekuwa tukitatua hizi changamoto, na hivi tunaenda kutengeneza Muswada mwingine wa ile Finance Bill ambayo kimsingi tunakuja kutatua changamoto ambayo kimsingi inawakumba sana wawekezaji wetu hususan wale wanaopewa vile vivutio kwa kupitia ile certificate of incentives.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, ni kweli wawekezaji wetu wa ndani hususan akina mama wa Mkoa wa Dodoma na vijana wakati fulani wanashindwa kushindana kwenye soko la uwekezaji, kwa sababu mbalimbali ikiwepo mitaji na kadhalika. Sisi kama Serikali, sasa hivi tunaenda kuandaa mwongozo mahususi wa incentives kwa ajili ya wazawa tu ambao utatupa way forward ni jinsi gani sasa tunaweza tukawafanya wakawa competitive na vilevile kuweka mazingira rafiki ya wao kupata mikopo na hata ardhi ili waweze kushindana na wawekezaji wanaotoka nje. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kuwasilisha.
Name
Asha Juma Feruz
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. NEEMA P. MAJULE aliuliza: - Je, Serikali imeweka vivutio gani vya uwekezaji kwa Wazawa ili kuwahamasisha kuwekeza zaidi nchini?
Supplementary Question 2
MHE. ASHA J. FERUZ: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipatia nafasi niulize swali la nyongeza. Je Serikali ina mkakati gani mahususi wa kuchukua hatua kwa wawekezaji ambao hawarudishi hii CSR katika maeneo yetu? Maana wapo wawekezaji ambao hawarudishi kabisa na wameshawekeza kwa muda mrefu?
Name
Dr. Pius Stephen Chaya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Asha Feruz, kwa kuwatetea wananchi ambapo wawekezaji wetu wameweka miundombinu au uwekezaji kule wa kupitia CSR (Corporate Social Responsibility). Ni kweli tunapokea changamoto kutoka kwa baadhi ya wawekezaji ambao hawa-comply na ile sheria yetu ya local content na tumekuwa tukishirikiana na Wizara za Kisekta, kwa sababu hii miradi ipo kwenye sekta mbalimbali; kwa watu wa ujenzi, kuna miradi kama hii, watu wa uchukuzi, watu wa kilimo na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi kama Serikali tupo on top of that na tutahakikisha tunashirikiana na Wizara nyingine ku-address haya matatizo tuhakikishe ile CSR sasa inalipwa kulingana na sheria ambayo imetungwa, ninashukuru.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved