Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Daniel Awack Tlemai
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karatu
Primary Question
MHE. DANIEL A. TLEMAI K.n.y. MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanzisha Mkoa wa Kikodi katika Wilaya ya Karatu? (Makofi)
Supplementary Question 1
MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa mwezi Oktoba, 2025, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwaahidi wananchi wa Jimbo la Karatu na kuwaambia, kwa maombi ya Wanakaratu sasa itakuwa Mkoa wa Kikodi. Kwa kuwa, Karatu ni eneo la katikati ya utalii kwa watalii wanaoelekea Ngorongoro, Manyara na Serengeti na mwaka 2024/2025 Serikali kupitia TRA, katika Wilaya ya Karatu, wamekusanya shilingi bilioni 11.12.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri imeonekana kwamba, Mkoa wa Kikodi wa Pemba wamekusanya shilingi bilioni 16 katika mwaka wa 2024/2025. Ukilinganisha inaonekana kwamba, inaweza kufananafanana kidogo, Karatu kuwa Mkoa wa Kikodi. Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya mwaka 2025 katika Jimbo la Karatu kwa wananchi wa Jimbo la Karatu? (Makofi)
Name
Mshamu Ali Munde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza kutoka kwa Mheshimiwa Daniel Awack Tlemai, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, kwa mujibu wa takwimu inaonyesha kwamba, shilingi bilioni 11.12 zimekusanywa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na inakaribia kabisa yale mapato ambayo yamekusanywa na Pemba ya shilingi bilioni 16. Ahadi za viongozi, ikiwemo ahadi ya Mheshimiwa Rais pamoja na maelekezo yake, ni vipaumbele vya Serikali kiutekelezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, wako kwenye threshold inavyoonekana, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Karatu, jambo hili kwa kuwa liko katika hatua za mwisho za tathmini, nina imani, na mimi nitasimamia uanzishwaji wa Mkoa wa Kikodi pale Karatu.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved