Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Nuru Issa Kashakari (1 total)

MHE. NURU I. KASHAKARI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Daraja la Mto Malagarasi, Kijiji cha Ilagara ili kuwasaidia wananchi wa ukanda wa Ziwa Tanganyika?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Nuru Issa Kashakari, Mbunge wa Kigoma Kusini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mto Malagarasi lililopo Kijiji cha Ilagala katika Barabara ya Simbo – Kalya (kilometa 231.29). Kwa sasa, Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.