Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Joshua Samwel Nassari (6 total)

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona, nina swali moja tu kwa upande wa Serikali. Wilaya kongwe ya Arumeru Makao Makuu yake ni Halmashauri ya Mji Mdogo wa Usa River. Fortunately, kwa miaka yote Halmashauri ya Mji Mdogo ule haina hata kilometa moja ya lami katika Mji wa Usa River. Tulitenga kilometa tano, na wananchi wakafanyiwa sensitization na Wizara kwa ile teknolojia mbadala ambayo imefanyika kwenye maeneo mengine, lakini unfortunately ile ya kwetu ya Meru haikujengwa kilometa tano pale Mji wa Usa River.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali. Ni lini jambo hili litakwenda kutekelezwa ili na yale maandamano ambayo mwaka 2025 kabla sijawa Mbunge yaliyowatoa wananchi wa Usa River kwenda kwa Mkuu wa Mkoa kwa sababu yasifanyike tena? Wananchi walishafanyiwa sensitization na kuachia maeneo yao na hakuna component ya fidia. Ni lini barabara hizi zitatekelezwa (five kilometers) kwenye Mamlaka ya Mji Mdogo wa Usa River? (Makofi)



NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikiri kwamba nimefika kwenye Jimbo la Mheshimiwa Mbunge, tuliambatana naye kwenda kufanya ukaguzi kwenye barabara ambayo tunaijenga kwa kiwango cha lami. Hivyo hivyo, kama ambavyo tumefanya jitihada kwenye barabara ile tuliyoikagua, tutaendelea kufanya jitihada kama Serikali kuhakikisha tunatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ili wananchi wa Arumeru na Makao Makuu ya Jimbo hilo Usa River waweze kupata huduma nzuri za barabara. (Makofi)
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru. Nitumie nafasi hii kuipongeza kwanza Wizara ya Maji kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya kwenye majimbo yetu huko, lakini nina swali moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa Uwilo pale Arumeru pamoja na Mradi mkubwa wa Maji wa Embaseni - Kikatiti pale Arumeru, ni lini Serikali itapeleka fedha ili wakandarasi waweze kurudi site na miradi hii iweze kuendelea kwa sababu tayari ilikwishaanza lakini imesimama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Nassari, Mbunge wa Arumeru, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Nassari kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya, lakini kubwa zaidi ushirikiano wake na Wizara ya Maji katika kubainisha changamoto zinazotokea katika jimbo lake. Tunamhakikishia kwamba, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan itapeleka fedha ili kuhakikisha miradi hii inakamilika na iweze kutoa matokeo na wananchi waweze kuona maji kwenye bomba hatimaye sasa nchi yetu isiwe na tatizo la water stress. Kwa hiyo, tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, hilo tunalichukua kwa makini sana. Ahsante sana.
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kuniona. Swali la msingi limeulizia habari ya soko na bei ya maziwa kwa wafugaji. Sasa Katika kukabiliana na tatizo hilo la soko na bei, wakulima na wafugaji wa Meru wameanzisha umoja wao unaitwa UWAWAME (Umoja wa Wakulima na Wafugaji Meru). Wanachohitaji kwa Serikali ili waweze kusaidika ni kuongeza thamani kwenye mazao ya maziwa na vitu vingine. Kuna baadhi ya vitu ambavyo wanahitaji msaada kutoka kwa Serikali kwa maana ya Wizara inayohusika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali iko tayari basi kukutana na hawa UWAWAME ili waweze kuwasaidia waweze kukabiliana na hii changamoto ya bei na soko kwenye maziwa?
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Ninamshukuru pia Mbunge kwa sababu mara kwa mara amekuwa akiniuliza juu ya namna gani tunaweza tukawafanya UWAWAME waweze kuendelea kuzalisha kwa tija zaidi hasa wafugaji katika umoja juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge katika muda na saa ambao tutapanga kwa pamoja na Wizara tupo tayari kukutana na UWAWAME ili twende tukaone namna gani ya kuwaongezea tija katika uzalishaji wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kuniona na mimi niulize swali dogo la nyongeza kwa Waziri wa Maji hapo. Kuna miradi mingi ya maji pale Arumeru, ambayo Serikali imeiasisi, lakini miradi ile imesimama kwa sababu ya kukosa fedha. Mathalani Mradi wa Imbaseni, Maji ya Chai, Kikatiti mpaka Maroroni, halikadhalika Mradi wa kule Uwiro, yote imesimama kwa sababu, certificates hazijalipwa. Je, Serikali inatoa commitment gani, ili wakandarasi waweze kurudi site?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Nassari, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza pamoja na kuuliza swali, Mheshimiwa Nassari tumekuwa tukizungumza sana mara kwa mara kuhusiana na suala hili. Kuna kipindi tulipanga ziara ya kwenda kuona namna gani tunaweza tukachukua hatua, ili miradi hii iweze kukamilika; lakini nimtoe hofu, miradi na wakandarasi wake tumeanza kufanya engagement, ili kuona namna gani tunakubaliana wakati tunashughulika kuhusu malipo ya hati zao za madai. Wao warudi site, ili kuhakikisha tusiwe na gap lolote hapa Katikati. Lengo ni kwamba, mradi ukamilike kwa wakati, na fedha zao waweze kulipwa wasije wakawa na changmoto yoyote ya kifedha. Ninakushukuru sana.
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kuniona na mimi niulize swali dogo la nyongeza kwa Waziri wa Maji hapo. Kuna miradi mingi ya maji pale Arumeru, ambayo Serikali imeiasisi, lakini miradi ile imesimama kwa sababu ya kukosa fedha. Mathalani Mradi wa Imbaseni, Maji ya Chai, Kikatiti mpaka Maroroni, halikadhalika Mradi wa kule Uwiro, yote imesimama kwa sababu, certificates hazijalipwa. Je, Serikali inatoa commitment gani, ili wakandarasi waweze kurudi site?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Nassari, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza pamoja na kuuliza swali, Mheshimiwa Nassari tumekuwa tukizungumza sana mara kwa mara kuhusiana na suala hili. Kuna kipindi tulipanga ziara ya kwenda kuona namna gani tunaweza tukachukua hatua, ili miradi hii iweze kukamilika; lakini nimtoe hofu, miradi na wakandarasi wake tumeanza kufanya engagement, ili kuona namna gani tunakubaliana wakati tunashughulika kuhusu malipo ya hati zao za madai. Wao warudi site, ili kuhakikisha tusiwe na gap lolote hapa Katikati. Lengo ni kwamba, mradi ukamilike kwa wakati, na fedha zao waweze kulipwa wasije wakawa na changmoto yoyote ya kifedha. Ninakushukuru sana.
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru nimepata access ya mic. Pia ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini niseme tu kwamba, sisi watu wa Wilaya ya Arumeru, ambao tupo chini ya Mlima Meru, nadhani siyo sawa sana kwamba, maji yanatoka kwetu yanakwenda Monduli, yanatoka kwetu yanakwenda Arusha Mjini na maeneo mengine, halafu sisi ambao tunatunza vyanzo vya maji bado kuna watu wetu hawana maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Waziri amesema hapo kwamba, miradi imesimama labda kwa kukosa fedha na nini, lakini kwa sababu ya flow ya fedha, kwa miradi ambayo Serikali imetoa fedha ila mkandarasi anasuasua, kwa mfano mkandarasi mkubwa wa Kikatiti – Samaria, mkandarasi anaitwa Help Desk, amepewa fedha, lakini bado anasuasua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumechunguza tukakuta huyo mkandarasi ana miradi mingi, kwa hiyo, ni kama vile anaelemewa. Halikadhalika, mradi mdogo wa hapo Imbaseni ambao unakwenda kutoa relief ambao upo chini ya Mamlaka ya AUWSA na wenyewe umefika mbali na Serikali imetoa fedha, lakini sijui kwa nini unasuasua kukamilika.

MWENYEKITI: Swali.

MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali yangu kwa Serikali. La kwanza, Serikali ipo tayari leo hii kufuatilia kwa hao watu wa AUWSA na yule bwana Help Desk, ili miradi ile iweze kukwamuka na kwenda mbele?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni ombi. Waziri wa Maji, ndugu yangu Mheshimiwa Juma Aweso hapo, ananisikiliza na ninajivuna kwamba mimi nilimpokea Form One Mwaka 2001 pale Bagamoyo Sekondari, na leo ni Mheshimiwa Waziri wetu wa Maji. Sasa, yupo tayari kuambatana na mimi ndugu yangu, twende kule Meru, ili tukaangalie miradi ya Uwiro, Shambarai na kwingineko, ambayo ni kama imesuasua, ili tuweze kuikwamua? Nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wa karibu. Ninakiri kwamba, tangu jana amekuwa akifuatilia, na leo hii amenijulia kabisa kwamba, atamwomba Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso, aongozanenaye na baada ya kuniambia nijibu moja kwa moja kwenye suala hilo, niliongea na Mheshimiwa Waziri akasema kwamba, yeye mwenyewe atanyanyuka kwenda mpaka katika Jimbo la Mheshimiwa Nassari kuhakikisha kwamba changamoto ambazo zinajitokeza katika eneo hilo, basi zinachukuliwa hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile picha nzima ya Arumeru Mashariki ni kwamba tunavyo vijiji 90, lakini katika vijiji 90 hivyo vijiji 52 vina huduma safi kabisa ya majisafi na salama. Tunatambua kwamba, kuna vijiji 30 ambavyo hali yake siyo ya kuridhisha sana. Tunafahamu pia, vijiji vinane hivyo ndivyo ambavyo havina mifumo rasmi ya utoaji wa huduma ya majisafi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamtoa hofu Mheshimiwa Mbunge, katika vijiji 1,575 vilivyobaki nchi nzima vijiji vyake vinane tutaviingiza katika programu hiyo, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, tunao mradi ambao umekamilika. Mradi wa Patandi ambao ni wa shilingi bilioni 3.125 tayari umeanza kutoa huduma ya majisafi na salama. Pia, Mradi wa Imbeseni tayari umeanza kutekelezwa. Tenki la lita 1,000,000 limekamilika, intake structure tumekamilisha na pia tunalaza mabomba. Kutoka kwenye chanzo kwenda kwenye bomba pale tumebakiza meta 500.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tunafamu kabisa kwamba, distribution line ambayo inatakiwa ni kilometa 14, kilometa nne tumekamilisha, sasa tupo kwenye hatua za mwishoni kuhakikisha kwamba, mradi huu unakamilika na wananchi wa maeneo ya Imbaseni wanapata huduma ya majisafi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na miradi mingine yote ambayo ipo, minane katika Jimbo la Mheshimiwa Nassari, ina gharama ya shilingi bilioni 10.147, ambapo ni uwekezaji mkubwa sana wa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nakushukuru sana.