Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Abdallah Jafari Chaurembo (1 total)

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Barabara ya kutoka Rangitatu, Majimatitu mpaka Mbande ni barabara ambayo imezidiwa sana na msongamano wa magari, kiasi kwamba mpaka bodaboda sasa zinapanga foleni. Je, Serikali ina mpango gani wa kuipanua barabara hiyo ili wananchi waweze kupita kwa urahisi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Jiji la Dar es Salaam, sehemu kubwa ina misongamano mikubwa. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshafanya study ya kuhakikisha kwamba sehemu zote ambazo zina changamoto zinajengwa upya, kwa maana ya kuongeza upana wa barabara ama kufanya njia nne.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Dar es Salaam, hasa wa maeneo ambayo ameyataja Mheshimiwa Chaurembo, nayo ni maeneo ambayo tayari yameshafanyiwa design, kwa maana ya kuijenga kwa njia nne ama kuipanua ili iweze kupunguza foleni ambayo ipo katika hayo maeneo.