Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Shaffin Ahmedali Sumar (2 total)

MHE. SHAFFIN A. SUMAR aliuliza:-

Je, Serikali inawasaidiaje wakulima wa tumbaku kupitia AMCOS kulipwa fedha jumla ya dola milioni 1.2 wanazodai kwenye kampuni?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Katika msimu wa 2024/2025 wakulima wa tumbaku waliuza kilo milioni 185.7 zenye thamani ya dola za Marekani milioni 475.45. Kati ya kiasi hicho, dola za Marekani milioni 470.95 sawa na 99.05% zimeshalipwa. Aidha, kiasi kinachodaiwa ni dola za Marekani Milioni 4.51 sawa na 0.95%. Kati ya kiasi kinachodaiwa, dola za Marekani 298,007.23 ni kutoka Wilaya ya Uyui.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kufuatilia madai ya wakulima wote wa zao la tumbaku ikiwemo wakulima kutoka Wilaya ya Uyui ili kuhakikisha madai yote ya wakulima wa zao la tumbaku hiyo yanalipwa kabla ya mwezi Machi, 2026.
MHE. SHAFFIN A. SUMAR aliuliza: -

Je, lini Serikali itafanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Bwawa la Maji na Chujio katika Kata ya Shitage?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Shaffin Ahmedali Sumar, Mbunge wa Jimbo la Uyui, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Bwawa la Maji la Shitage katika Kijiji cha Shitage Kata ya Shitage Wilayani Uyui Mkoa wa Tabora. Mara baada ya ujenzi wa bwawa hilo kukamilika, usanifu wa miundombinu ya usambazaji maji ukijumuisha mtambo wa kuchuja na kutibu maji utafanyika. Ninakushukuru.