Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Said Ali Mbarouk (1 total)

MHE. RASHID HABIB ALI K.n.y. MHE. SAID ALI MBAROUK aliuliza:-

Mpango gani wa kuondoa utaratibu wa sasa wa kikokotoo kwa Wastaafu wa Jeshi la Polisi, ili kuboresha maslahi kwa Wastaafu?
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA MAHUSIANO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Said Ali Mbarouk, Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya Serikali ni kuendelea kuboresha mafao ya wastaafu wote, ikiwemo wa Jeshi la Polisi, kadiri mifuko ya pensheni inavyoimarika na si kuondoa utaratibu uliopo sasa unaotumika kulipa mafao. Mifuko ya pensheni inatumia kanuni maalum au kikokotoo katika kulipa mafao kwa wanachama wanaochangia katika mifuko hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni hii hutumika kwa wafanyakazi wote walioajiriwa katika sekta ya umma na binafsi, ikiwemo Jeshi la Polisi. Aidha, Kanuni hii hairuhusu kuwa na ukokotoaji tofauti katika mfuko wa pensheni kwa wanachama wenye sifa zinazofanana. Nninaomba kuwasilisha.