Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Simai Mohammed Said (1 total)

MHE. SIMAI MOHAMMED SAID: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina swali dogo tu la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kila mwaka Serikali inakuja katika Bunge lako Tukufu katika kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali. Ni utaratibu upi Serikali inatumia katika kupima au kujua ni vipaumbele gani wafanyabiashara wanapata katika kuwapatia mikopo ndani ya Tanzania?

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania pia tumepakana na nchi nane kama tutachukua pamoja na Comoros itakuwa ya tisa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, swali la nyongeza ni moja. Haya Mheshimiwa jibu swali la nyongeza.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA): Mheshimiwa Naibu Spika, sijamsikia vizuri.

NAIBU SPIKA: Hajasikia swali la nyongeza hilo la kwanza. Ni vigezo gani vinatumika kwenye…

MHE. SIMAI MOHAMMED SAID: Mheshimiwa Naibu Spika, ni utaratibu upi Serikali inatumia tunapokuja kila mwaka hapa katika kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali, ili na sisi Wabunge pia tujue? Kwa mfano, kila mwaka Serikali inakuja Bungeni katika kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali na sisi Wabunge tunataka tuunge mkono vipaumbele vya Serikali. Ni utaratibu upi Serikali inatumia katika kupima jinsi gani hii mikopo tunaweza kuwapatia wafanyabiashara katika maeneo tofauti ndani ya Tanzania? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge, nimwombe na nikiombe Kiti chako kama itampendeza Mheshimiwa Mbunge alilete swali hili kama swali la msingi na sisi kama Wizara ya Fedha tutalipatia majibu ya kutosha na toshelezi. Ahsante sana. (Makofi)