Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Asha Juma Feruz (1 total)

MHE. YUMNA MMANGA OMAR K.n.y. MHE. ASHA J. FERUZ aliuliza:-

Je, Serikali imewaunganishaje wahitimu wa kada zinazoendana na utekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini?
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA MAHUSIANO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu wali la Mheshimiwa Asha Juma Feruz, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa inatumia miradi mikubwa ya kimkakati kuwaunganisha wahitimu wa kada mbalimbali na fursa za miradi hiyo, kama sehemu ya kuzalisha ajira na kuwapa uzoefu wahitimu hao. Takribani ajira 35,000 zimezalishwa katika ujenzi wa Mradi wa SGR, 10,000 katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi (EACOP), 10,000 katika ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere, ajira 1,500 katika ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, ajira 1,500 katika ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi na 3,000 katika upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua nyingine ni kuhusisha na kuimarisha programu za mafunzo ya uzoefu wa kazi (internship), ili wahitimu waweze kupata uzoefu unaoendana na mahitaji ya waajiri. Hadi Aprili, 2026 jumla ya wahitimu 29,902 walikuwa wamepata mafunzo hayo. Aidha, Serikali imeandaa Mwongozo wa Taifa wa Mafunzo kwa Vitendo kwa Wahitimu wa mwaka 2017 unaotumika katika sekta ya umma na binafsi. Vilevile, kuwajengea uwezo vijana na wafanyakazi katika maeneo yenye mahitaji makubwa ya kitaaluma na kiufundi. Hadi kufikia Aprili, 2026 Watanzania 168,657 walikuwa wamenufaika na programu hiyo. Ninaomba kuwasilisha.