Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Kijakazi Mohamed Yunus (1 total)

MHE. KIJAKAZI Y. MOHAMED aliuliza: -

Je, lini Mkataba wa kuchakata Gesi Asilia (LNG) Lindi utasainiwa na kuanza utekelezaji?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Kijakazi Yunus Mohamed, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali na wawekezaji wa mradi wa kuchakata gesi asilia (LNG) Mkoani Lindi wapo katika hatua ya mwisho ya majadiliano, hususan kwenye masuala ya kisheria ili kuwezesha usainishaji wa mikataba na makubaliano, na hatimaye utekelezaji wa mradi kuanza. Aidha, wabia wa mradi wameendelea na miradi ya kijamii ikiwemo ujenzi wa Shule ya Msingi Mpya ya Likong’o ambayo ujenzi wake umefikia 90%.