Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 3 | Sitting 23 | Questions to Prime Minister | Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji | 1 | 2016-05-19 | 
 
									Name
Freeman Aikaeli Mbowe
Gender
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Hai
Primary Question
						MHE.  FREEMAN  A.  MBOWE:
Mheshimiwa  Spika,  nakushukuru  kunipa  nafasi ya kumuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu maswali. 
Mheshimiwa  Waziri Mkuu  unatambua  kwamba  sasa  hivi  nchi  ina  uhaba mkubwa wa sukari. uhaba huu wa sukari umesababishwa na amri iliyotolewa na Mheshimiwa  Rais  mwezi  Februari  mwaka  huu  ya  kuzuia  uagizaji  wa  sukari  bila kufuata utaratibu ama kufanya utafiti wa kutosha kuhusiana na tatizo zima ama biashara nzima ya uagizaji na usambazaji wa sukari katika Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa   Waziri   Mkuu,   tunatambua   kwamba   nchi   yetu   inazalisha takribani wastani wa tani milioni 300 na zaidi ya tani 180 hivi zinaagizwa kutoka nchi  za  nje  na  sasa  hivi  wewe  mwenyewe  umetoa  kauli  kwamba  Serikali imeagiza sukari. 
Sasa swali langu ni hili; maadam sukari ina utaratibu maalum  wa uagizaji ambao  unasimamiwa  na  Sheria  ya  Sukari  ya  mwaka  nafikiri Sugar  Industry  Act ya mwaka 2001 na kwamba Bodi ya Sukari inatoa utaratibu maalum wa uagizaji wa sukari hii na biashara ya uagizaji sukari sio tu uagizaji kwa sababu ya fedha ni  pamoja  na  muda  maalum, circle maalum  wakati  gani  agizo  hili  isingane  na uzalishaji katika viwanda vya ndani ambavyo Mheshimiwa Rais alidai alikuwa na 
nia ya kuvilinda ambalo ni jambo jema.
Mheshimiwa    Waziri    Mkuu,    sasa    unaweza    ukatuambia    hiyo    sukari uliyoagiza umeiagiza kwa utaratibu gani? Anaiagiza nani? Inategemewa kufika lini?  Ni  kiasi  gani?  Na  itakapofika  haitagongana  na  uzalishaji katika  viwanda vyetu local baada ya kuisha kwa msimu wa mvua na hivyo kusababisha  tatizo la sukari kwa mwaka mzima ujao? 
					
 
									Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
						WAZIRI   MKUU:
Mheshimiwa   Spika,   kwanza   nimshukuru   Mheshimiwa Mbowe,  Mbunge  wa  Hai  na  Kiongozi  wetu  wa  Kambi  ya  Upinzani  kwa  kuuliza swali   hili   kwa   sababu   tulitaka   tutumie   nafasi   hii   kuwaondoa   mashaka Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa  Spika,  Mheshimiwa  Rais  wakati  wote  anapotoa  tamko  ni kutokana na mwelekeo na mpango wa Serikali ambao umepangwa kwa lengo maalum.  Sukari  nchini  ni  k
weli  kwamba  inaratibiwa  na  Bodi  ya  Sukari  ambayo pia imewekwa kisheria na moja kati ya majukumu yao kufanya utafiti, lakini pia kusimamia  viwanda  vinavyozalisha  kwa  lengo  la  kusambaza  sukari  nchini  na iweze kutosha.
Mheshimwia  Spika,  kwa  miaka  mitatu,  minne  ya  nyuma,  sukari  imekuwa ikiletwa   kwa   utaratibu   ambao   baadaye   tuligundua   kwamba   unavuruga mwenendo  wa  viwanda  vya  ndani  na  viwanda  vya  ndani  havipati  tija.  Kwa hiyo,   Serikali   hii   ilipoingia   madarakani   moja   kati   ya   mikakati   yake   ni kuhahakikisha  kwamba  viwanda  vya  ndani  vinalindwa,  unavilindaje?  Ni  pale ambako  sasa  sukari  inayoingia  ndani  lazima  idhibitiwe  lakini  pia  kuhamasisha viwanda hivyo kuzalisha zaidi sukari. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mahitaji ya sukari nchini ni tani 420,000. Sukari ambayo inazalishwa nchini ni tani 320,000 na upungufu ni kama 100,000 hivi. Tani 100,000 hii  kama  hatuwezi  kuiagiza  kwa  utaratibu  na  udhibiti  mzuri  kunaweza  kuingia kwa  sukari  nyingi  sana  kwa  sababu  kwenye  sukari  tuna  sukari  za  aina  mbili, sukari ya mezani ile ambayo tunaitumia kwenye chai na sukari ya viwandani na haina  utofauti  mkubwa  sana  kwa  kuingalia  na  sukari  ya  viwandani  na  ya 
mezani  ni  rahisi  sana  kwa  mwagizaji  kama  hatuwezi  kudhibiti  vizuri  unaweza kuleta sukari nyingi ya mezani halafu kukajaa sokoni.Mheshimiwa  Spika,  kwa  hiyo  kauli  ya  Mheshimiwa  Rais  ni  katika  mpango wa  kulinda  viwanda  vya  ndani  kama  ambavyo  umekiri,  lakini  jukumu  la  Bodi sasa  ya  Sukari  baada  ya  kauli  ile  inatakiwa  sasa  iratibu  vizuri.  Kwa  hiyo,  sukari imeratibiwa  vizuri  na  bodi  ya  sukari  na mahitaji  ya  sukari  ile  ya  tani  100,000  na 
mahitaji  ya  sukari  ambayo  inatakiwa  kuingia  ili  isivuruge  uzalishaji  ujao  ni  kazi ambayo inafanywa Bodi ya Sukari. 
					
 
											Name
Freeman Aikaeli Mbowe
Gender
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Hai
Question 1
MHE.  FREEMAN  A.  MBOWE: 
Mheshimiwa  Spika,  Mheshimiwa  Waziri  Mkuu nakushukuru   kwa   ajibu   yako   na   ninaomba   nikuulize   maswali   mengine machache ya ziada. 
Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na nia njema sana ya kulinda viwanda 
vya  ndani  ni  dhahiri  kwamba  maamuzi  yote  ya  kiutawala  lazima  yafanyiwe kwanza   utafiti.   Na   tunapozungumza   ninahakika   Serikali   yako   inatambua kwamba  kuna  mradi  mkubwa  wa  uwekezaji  wa  kiwanda  cha  sukari  uliokuwa umependekezwa  katika  eneo  la  Bagamoyo  uliouzungumza  ambao  umeanza kuratibiwa  tangu  mwaka  2006  wenye capacity ya  kuzalisha  sukari  tani  125,000 kwa   mwaka,   lakini   Serikali   mpaka   dakika   hii   tunapozungumza   urasimu unasababisha mradi huu haujapewa kibali cha kuanza. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu, pamoja na kwamba ulisema kuna bei ya 
elekezi sukari ambayo ingehitaji soko la sukari liweze kuwa controlled na Serikali, jambo  ambalo  linaonekana  kushindikana.   Unatupa  kauli  gani   Watanzania kuhusiana sasa na hatima ya hayo mambo niliyokuuliza? 
 
											Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
								WAZIRI    MKUU: 
Mheshimiwa    Spika,    naomba    kujibu    swali    pana    la Mheshimiwa  Mbowe,  Mbunge  wa  Hai  na  Kiongozi  wa  Kambi  ya  Upinzani Bungeni kama ifuatavyo:-
Kwanza  tuna  hilo  shamba  la  Bagamoyo  ambalo  umelisema  ambalo 
umesema  kumekuwa  na  urasimu  wa  muda  mrefu.  Nataka  nijibu  hili  vizuri  kwa sababu  pia  Wabunge  tumeshirikiana  nao  sana  katika  kufanya  maamuzi  ya shamba lile. (Makofi)
Mheshimiwa   Spika,   shamba   la   Bagamoyo   kwa   ukubwa   wake   na 
mategemeo  yake  kwa  mipango  ya  kuzalisha  sukari  inategemea  sana  Mto Wami.  Mpakani  mwa  Mto  Wami  tumepakana  na  Mbuga  ya  Saadani,  Mbuga ya  Saadani  uwepo  wake  na  sifa  iliyonayo  inategemea  sana  wanyama  wale kunywa maji Mto Wami. (Makofi)
Mheshimiwa  Spika,  uwekezaji  wa  shamba  la  sukari  unahitaji  maji  mengi nayo  yanatakiwa yatoke Mto  Wami. Bado kuna mgongano kidogo wa mpaka kati  ya  shamba  letu  hilo  la  sukari  linalotegemewa  kulima  miwa  na  Mbuga  ya Saadani.  Kamati  ya  Kudumu  ya  Bunge  imefanya  ziara  na  imeishauri  Serikali kuangalia  vinginevyo  na  mimi  nimepokea  ushauri  wao  vizuri  kwa  sababu  una mantiki. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bunge imeishauri Serikali kwamba ni vyema 
tukahifadhi mbuga, tukatafuta maeneo mengine ya kilimo cha sukari ili kulinda Mto  Wami  ambao  unatumiwa  na  wanyama  wetu  kwenye  Mbuga  ya  Saadani kuliko kupeleka shamba tukatumia maji yale tukafukuza wanyama hakutakuwa na mbuga tena.
Mheshimiwa   Spika,   sisi   bado   tuna   nafasi   kubwa   ya   maeneo   mengi ambayo  yamefanyiwa  utafiti  ya  kulima  sukari,  mbali  ya  eneo  la  Morogoro  na kule Kigoma, lakini tuna eneo la shamba lililokuwa linamilikiwa na Bodi ya Sukari kule Kilombero, nalo pia lina nafasi nzuri tu tunaweza kuzungumza na wakulima wanaolima mashamba ya kawaida watuachie tuweze kuwekeza.
Mheshimiwa Spika, lakini tuna Mto Rufiji tuna bonde kubwa sana uliokuwa 
unamilikiwa na watu wa Bonde la Rubada, wana eneo kubwa sana. Kwa hiyo, tuna  maeneo  hayo mengi,  tutakapopata  wawekezaji  wengi  tutaanza  kupima viwanda   vilivyopo   na   uzalishaji   wake.   Makubaliano   ya   kiwanda   kipya   na uzalishaji wake tukigundua kwamba, uzalishaji wake unatosha mahitaji ya nchi. 
Tutaanza    kuwakabidha    Kigoma,    tutawepeleka    Morogoro    kule    Kilosa, tutawapeleka hapa Ngerengere na Bagamoyo iwe sehemu ya mwisho baada ya  kuwa  Kamati  ya  Bunge  imetushauri  vizuri  juu  ya  kulinda  Mbuga  yetu  ya Saadani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, eneo la pili, ambalo umelitaja ni hili la bei elekezi, kwa 
nini tunatoa bei elekezi. 
Mheshimiwa Spika, mara nyingi tunakaa sana na wazalishaji wa viwanda 
wa  sukari  na  kufanya  mapitio  na  kwa  mara  ya  mwisho  tumekutana  hata  wale waagizaji  wa  muda  mrefu  na  sasa  tunajua  kupitia  mitandao  tunajua  bei wanayonunulia  sukari  huko  ughaibuni.  Brazil  na  kule  Uarabuni  tumeshafanya calculation za pamoja mpaka sukari inaingia nchini na kulipa kodi zake.
Mheshimiwa Spika, usafirishaji kutoka Dar es Salaam na kuipeleka mpaka 
mkoa  wa  mwisho  Kagera,  Lindi,  Ngara,  tunajua  kule  Ngara  itauzwa  bei  gani. 
Kwa  hiyo,  wajibu  wa  Serikali  kutoa  bei  dira  ni  kumlinda  sasa  mwananchi  wa kawaida  asije  auziwe  kwa  gharama  kubwa  kwa  kisingizio  cha  usafirishaji  huku tukiwa  tunajua  usafirishaji  kutoka  Brazil  mpaka  Dar  es  Salaam,  Dar  es  Salaam mpaka Ngara na mwananchi wa Ngara atanunua sukari kwa kiasi gani.
Mheshimiwa  Spika,  kwa  hiyo  suala  la  bei  elekezi  litategemea  linaweza 
likabadilika   kutegemea   na   gharama   ya   usafirishaji   ambayo   na   sisi   pia tunafuatilia  kwa  karibu  kupitia  Bodi  yetu  ya  Sukari.  Kwa  hiyo,  suala  bei dira linaweza  kubadilika  na  sisi  tunatoa  kauli  kutegemea  na  uagizaji  lakini  lazima wananchi waamini kwamba Serikali hii inawalinda walaji wadogo ili wasinunue sukari kwa bei ya juu.