Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 3 | Sitting 23 | Water and Irrigation | Maswali kwa Waziri Mkuu | 3 | 2016-05-19 | 
 
									Name
Hassan Selemani Kaunje
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Lindi Mjini
Primary Question
						MHE.  HASSAN  S.  KAUNJE:
Mheshimiwa  Spika,  nishukuru  kupata  nafasi  ya kuuliza swali la moja kwa moja kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. 
Mheshimiwa  Waziri  Mkuu,  kwanza  tunafahamu  kwamba  maji  ni  uhai  na Sera  ya  Taifa  ya  Maji  inahitaji  kila  mwananchi  kuweza  kuyafikia  maji  ndani  ya umbali wa mita 25. Je, Serikali ya Awamu ya Tano imejipangaje kuhakikisha maji haya  yanawafikia  wananchi especially
wananchi  wa  Mkoa  wa  Lindi  ambao wanatatizo kubwa sana la maji?
					
 
									Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
						WAZIRI  MKUU:
Mheshimiwa  Spika,  naomba  kujibu  swali  la  Mheshimiwa Kaunje, Mbunge wa Lindi Mjini kama ifuatavyo:-
Kwanza  nimpongeze  Mheshimiwa  Kaunje,  amekuwa  anafuatilia  sana mwenendo wa maji na hasa alipoweka kule mwishoni hasa wananchi wa Mkoa wa Lindi. (Makofi)
Mheshimiwa  Spika,  ni  kweli  kwamba  Sera  ya  Maji  nchini  imetamka  wazi kwamba Serikali itasambaza maji kwa wananchi wake kote nchini mpaka ngazi za  vijiji  tena  kwa  umbali  usiozidi  mita  400  hiyo  ndiyo  sera  na  wakati  wowote Wizara  ya  Maji  inapofanya  kazi  yake  inafanya  kazi  kuhakikisha  kwamba  sera hiyo inakamilika. Iko mipango mbalimbali na nadhani Wizara ya Maji itakuja na bajeti   hapa   ikiomba   ridhaa   yenu   muipitishe   Waheshimiwa   Wabunge   ili tukaendelee kutekeleza hiyo sera ya kusambaza maji, na mikakati yetu sisi, maji 
lazima  yawe  yamefika  kwenye  ngazi  za  vijiji  kwa  asilimia  mia  moja  ifikapo mwaka 2025 na ikiwezekana kufikia mwaka 2020 hapa kwa zaidi ya asilimia tisini huo  ndiyo  mkakati  wetu.  Mkakati  huu  utatokana  tu  kama  tutaendelea  kupata fedha nyingi Serikalini na kuzipeleka Wizara ya Maji ili Wizara ya Maji waendelee na mkakati ambao wanao.
Kwa    hiyo,    niseme    tu    kwamba    kwa    malengo    haya    tunakusudia kusambaza  maji  kwenye  maeneo  yote  ya  vijiji  na  maeneo  ya  miji  ili  wananchi wetu  waweze  kupata  tija  ya  maji  kwenye  maeneo  haya.  Kwa  miradi  ambayo ipo,   ambayo   imeelezwa   kwamba   ipo   inaendelea   kutekelezwa,   tunaamini miradi   hiyo   kwa   watu   wote   ambao   tumewapa   kazi   hiyo   wataendelea kutekeleza   kadri   ambavyo   tunawalipa   fedha   zao   ili   waweze   kukamilisha. 
Waliokamilisha   wakamilishe    miradi    ambao    hawajakamilisha    tunaendelea kuwapelekea  fedha  ili  waweze  kukamilisha  ili  maji  yaweze  kutolewa  na  kila mwananchi aweze kunufaika na sera hiyo ya Serikali.
					
 
											Name
Hassan Selemani Kaunje
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Lindi Mjini
Question 1
MHE.  HASSAN  S.  KAUNJE:
Mheshimiwa  spika,  ahsante  sana.  Mheshimiwa Waziri  Mkuu,  sababu  zinazosababisha  muda  mwingine  kutokupatikana  maji  ni pamoja  na  wakandarasi  ambao  wanakuwa  wamelipwa  lakini  wanashindwa 
kukamilisha miradi ya  maji  kwa wakati  na  sababu  hizo  ni  pamoja  na  mradi wa Ng‟apa ambao uko Lindi. Je, ni hatua gani zinachukuliwa na Serikali dhidi ya wakandarasi wa aina hii ili maji yaweze kuwafikia wananchi?
 
											Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
								WAZIRI  MKUU:
Mheshimiwa  Spika,  naomba  kujibu  swali  la  nyongeza  la 
Mheshimiwa Kaunje, Mbunge wa Lindi Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa  Spika,  kama  ambavyo  nimeeleza  kwenye  jibu  langu  la 
msingi,  suala  la  wakandarasi  wetu  kwa  sababu  malengo  ya  Serikali  tunawapa hizi   kazi   ili   waweze   kuzimaliza   katika   kipindi   kifupi   sasa   kama   inatokea mkandarasi  hawezi  kamaliza  kazi  kwa  kipindi  kifupi,  ziko  sababu  mbalimbali ambazo pia tumezizoea maeneo mengine, malipo kutoka kwa kuchelewa nako kutokana   na   tatizo   la   fedha   inawezekana mkandarasi   hajamaliza.   Lakini malengo  yetu  kama  mkandarasi  analipwa  vizuri  na  kwahiyo  basi  anatakiwa akamilishe   mradi   huo   kwa   wakati   uliokubalika.   Lakini   ikitokea   mkandarasi 
hajamaliza  kama  kuna  tatizo  la  fedha  hilo  ni  juu  ya  Serikali  kupitia  Wizara  ya Fedha   kukamilisha   kulipa   madeni   ili   mradi   ukamilike.   Kama   mkandarasi amelipwa  fedha  zote  au  zaidi  ya  asilimia  90    na  hajakamilisha  kwa  kipindi kinachotakiwa,  zipo  taratibu  za  kisheria  za  kufanya  kwa  sababu  ameingia zabuni kisheria na kwa hiyo,  tunaweza tukatumia utaratibu wa kisheria pia kwa kuadhibu mkandarasi ambaye hajamaliza kazi lakini pia amelipwa fedha. 
Sasa  sina  uhakika  na  mradi  wa  Lindi  uko  katika  sura  gani  na  kama 
ingekuwa session hii inaweza kumpa Waziri Mkuu nafasi ya kupata majibu sahihi ningweza kukupa jibu sahihi la mradi huo wa Ng‟apa.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved