Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 3 | Sitting 23 | Industries and Trade | Maswali kwa Waziri Mkuu | 4 | 2016-05-19 | 
 
									Name
Lucy Simon Magereli
Gender
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
						MHE. LUCY S. MAGERELI:
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la moja kwa moja kwa Waziri Mkuu. 
Mheshimiwa   Waziri   Mkuu ,   Mpango   wa   Serikali   wa   Miaka   Mitano   ni kuipeleka Tanzania kuwa Tanzania ya viwanda na ziko changamoto zinazokabli mpango  huo  na  moja  ni  namna  ya  kuwawezesha  wazalishaji  na  wafungashaji wadogo  katika level za  Halmashauri  kufanya  kazi  hiyo  kwa  ufanisi  mkubwa. 
Tunafahamu  uwepo  wa GS1 ambayo  inalengo  la  kuwasaidia  wazalishaji  na wafungashaji hao kupata barcodes ili waweze kuuza bidhaa zao. Mwaka jana Waziri  Mheshimiwa  Mizengo  Pinda  alitoa  maelekezo  ya  maandishi  akielekeza TAMISEMI   iagize   halmashauri   zote   zitoe
ushirikiano   kwa GS1 ili   waweze kuwasaidia  hao  wazalishaji  na  wafungashaji  wadogo  kupata barcodes kitu ambacho kinge-stimulate uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo...
SPIKA:
Mheshimiwa Lucy sasa swali.
MHE.   LUCY   S.   MAGERELI: 
Mheshimiwa   Spika   ahsante,   ningetemani nimalizie, anyway.
Nini sasa Kauli ya Serikali hasa kwa Ofisi  ya  Waziri Mkuu  katika kusimamia na  kutekeleza  maelekezo  haya  ambayo  tayari  yalishatolewa  na  Ofisi  ya  Waziri Mkuu aliyepita ili kuwasaidia wazalishaji na wafungashaji wadogo hawa?
					
 
									Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
						WAZIRI  MKUU:
Mheshimiwa  Spika,  naomba  kujibu  swali  la  Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Ni   kweli   kwamba   Serikali   inayo   mkakati,   tunaendelea   kuhamasisha wajasiriamali  wadogo  kujiendeleza  kupitia  viwanda  vidogo  vidogo  na  msisitizo huu wa Serikali wa viwanda unajumuisha viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kwa  lengo  lile  lile  la  kumtaka  Mtanzania  aweze  kunufaika  na  hasa  katika kuongeza thamani ya mazao ambayo tunayazalisha nchini. 
Tumeendelea  kuwa  na  mipango  mbalimbali  ambayo  Serikali  inaunga mkono   jitihada   za   wazalishaji   wadogo   ikiwemo   na   uwekaji   wa barcodes ambayo  pia  inamsaidia  kupata  bei  na    thamani  nzuri  ya  mazao  ambayo mjasiriamali  anajihusisha  katika  kuchakata  kwenye  michakato  ya  awali  kwa maana processing hii ya awali. 
Mheshimiwa   Spika,   mkakati   huu   bado   unaendelea   na   tumeagiza utaratibu   huu   wa 
barcodes uendelee   lakini   pia   tumehusisha TBS,   TFDA kuhakikisha  kwamba  chakula  tunachokizalisha  kinakuwa  na  ubora  ili  tukikipa barcode, Taifa liweze kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi na ndani ya nchi ambako tunaweza kupata fedha nyingi na wajasiriamali waweze kunufaika zaidi.
Kwa   hiyo,   nataka   nikuhakikishie   tu   kwamba   utaratibu   huo   bado unaendelea ili kuweza kuipa thamani mazo yetu lakini kuwapa uwezo mkubwa wa   kusafirisha   bidhaa   zao   nje   na   kuzipa   soko   ili   ziweze   kuwaletea   tija Watanzania   na   tutaendelea   pia   kusimamia   jambo   hilo   kuwa   linaendelea kukamilika. Ahsante sana.
					
 
											Name
Lucy Simon Magereli
Gender
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Question 1
MHE. LUCY S. MAGERELI: 
Mheshimiwa Spika, nakushukuru. 
Mheshimiwa  Waziri  Mkuu,  nilichotamani  kusikia  kutoka  kwako  ni  tamko lako  kama  Serikali  kuziagiza  Halmashauri  kutoa  ushirikiano  kwa 
GS1 lakini TFDA, TBS na  washirika  wengine  ikiwemo  Wasajili  wa  Viwanda  wa  Makampuni  kwa sababu  hiyo  ni  timu  inayofanya  kazi  pamoja.  Changamoto  hiyo  imekuwa kubwa  kwa  sababu  ya  kupata 
resistance kutoka  kwa  Halmashauri,  lengo mlilolianzisha  lilikuwa  jema  lakini  Halmashauri  hazitoi  ushirikiano  na  kutotoa ushirikiano zinawanyima fursa wazalishaji na wafungashaji wadogo kupata fursa hiyo.
 
											Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
								WAZIRI  MKUU:
Mheshimiwa  Spika,  naomba  kujibu  swali  la  nyongeza  la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa  Spika,  nimekusikia  kwa  namna  ambavyo  ume-experience
huko  ambako  umeona  kwamba  Halmashauri  zetu  hazitekelezi  maagizo  yetu ambayo  tunayatoa  na  inawezekana  siyo  Halmashauri  tu  ziko  pia  nyingine ambazo  pia  zinafanya  jambo  hilo  hilo.  Kwa  hiyo,  nilichukue  jambo lako  baada ya kikao hiki nitawasiliana na Waziri wa TAMISEMI kuhakikisha kwamba maagizo yetu ya Serikali yanatekelezwa na wazalishaji wetu wadogo wanapata nafasi. 
Lakini  pia  Wizara  ya  Kilimo  nayo  pia  ilichukue  hili  kwa  sababu  tunayo 
Maonesho  ya  Kilimo  ambayo  sasa  tumeyaanzisha  katika  kanda  mbalimbali, hawa  wajasiriamali  wadogo  wapate  nafasi  za  kwenda  kuonyesha  bidhaa  zao kwenye maonyesho yale ili pia waweze kutangaza soko lao, waonyeshe ubora wao na sasa Halmashauri zisimamie wajasiriamali wadogo hao kwenda kwenye maonyesho  hayo  ili  uonyesha  kazi  zao  ziweze  kuleta  tija  zaidi  huo  ndiyo msisitizo wa Serikali. 
(Makofi)
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved