Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 3 | Sitting 23 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Maswali kwa Waziri Mkuu | 5 | 2016-05-19 | 
 
									Name
Ester Alexander Mahawe
Gender
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
						MHE. ESTER A. MAHAWE: 
Mheshimiwa Spika, ahsante. 
Mheshimiwa  Waziri  Mkuu,  sera  ya  elimu  ya  nchi  yetu  sasa  inasema  ni kupata   elimu   bure   lakini   hii   bure   ina   maana   inalipiwa   na   Serikali.   Lakini kumekuwa  na  kundi  dogo  la  wazazi  wengine  ambao  kwa  kuchangia  kupitia kodi  zao  ndizo  ambazo  zinatumika  kusomesha  watoto  wao  ama  kugharamia elimu  lakini  kundi  hili  limekuwa  likilipa  kodi  zote  zinazotakiwa  kulipwa  lakini wamekuwa  wakichajiwa  mara  mbili (double  taxation) kupitia  watoa  huduma wa elimu katika taasisi binafsi. 
Je,  nini  kauli  ya  Serikali  ili  kwamba  na  hawa  wananchi  amba  tayari walikwisha kulipa kodi na kuchangia elimu bure na wenyewe waweze kufurahia keki hii ya elimu bure? (Makofi)
					
 
									Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
						WAZIRI  MKUU:
Mheshimiwa  Spika,  kama  ambavyo  umesema,  kwamba swali limechanganywa sana haliko wazi mno na haya ni maswali ya papo kwa papo inatakiwa liwe-clear ili na mimi niweze kujibu  kitu halisi  ili pia naye  aweze kunufaika   na   majibu   lakini   pia   Watanzania   ambao   wanasikia   kipindi   hiki waweze   kujua   jambo   gani   limeulizwa   na   jambo   gani   ambalo   linatakiwa kujibiwa. 
Lakini  pia,  amezungumzia  suala  la  elimu  bure  na  ni  jambo  ambalo  watu wengi   limekuwa   likiwachanganya   na   wengine   kupotosha,   naomba   nitoe ufafanuzi  huu  ufuatao  ili  Watanzania  wajue  kwamba  elimu  bure  ni  mkakati unaolenga  Kurugenzi  ya  Msingi  na  Sekondari  na  hasa  katika  kuwapunguzia mzigo wazazi wa kuchangia changia michango mbalimbali shuleni. 
Mheshimiwa  Spika,  Serikali  tumeanza  na  maeneo  ambayo   tumeona wazazi   walikuwa   wanakwazwa   sana.   Tumezungumza   mara   kadhaa   lakini narudia   kwamba   moja   kati   ya   maeneo   hayo   tumeondoa   yakle   malipo yaliyokuwa  yanaitwa  ada  kwa  sekondari,  shilingi  20,000  na  shilingi  70,000.  Pia kulikuwa na michango ya ulinzi, maji, umeme pale shuleni michango ile yote ile sasa  Serikali  imetenga  fungu  kwa  ajili  ya  kuipa  shule  ili  iweze  kulipia  gharama hizo,  lakini  suala  la  mitihani  mbalimbali  nayo  pia  ni  eneo  Serikali  imeamua kulichukua  kwa  sababu  gharama  za  mitihani  zitafanywa  na  Serikali  ili  wazazi 
wasiingie kwenye michango hiyo. 
Mheshimiwa   Spika,   lakini   pia   tunaendelea   kuona   ni   maeneo   gani mengine  ambayo  wazazi  yanawakwaza  zaidi  katika  kuchangia,  sasa  kama kuna mzazi anachangia huku nje hata kama analipa kodi maeneo mengine, ni jukumu  tu  la  kuona  kwamba  kuna  umuhimu  wa  kuchangia  sekta  ya  elimu  na kwamba yeye kama Mtanzania anayo nafasi ya kuchangia mahali popote bila kujali  kama  mchango  huo  pia  unagusa  kodi  ambazo  alikuwa  anazilipa  kule awali.
Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, tutoe wito kwa Watanzania, kwanza tupe    subira    Serikali    kuona    maeneo    mengine    zaidi    ambayo    tunaweza tukaboresha ili kumpunguzia mzazi mzigo wa kuweza kusomesha watoto hawa. 
Sasa  lawama  inakuja  pale  ambako  tumetoa  nafasi  hizi  tumegundua kwamba  kuna  watoto  wengi  wa  Kitanzania  walikuwa  hawapelekwi  shuleni  na kwa  kuondoa  hizi  gharama,  gharama watoto  wengi  wanapelekwa  shule  na sasa   tumeanza   kuona   uzoefu   wa   kwamba   watoto   wengi   wameendelea kusajiliwa   shuleni,   idadi   imekuwa   kubwa   na   kumekuwa   na   changamoto nyingine kama madawati na vyumba vya madarasa.(Makofi)
Mheshimiwa  Spika,  nataka  niwahakikishi e  Watanzania,  kwamba  Serikali inaendelea  kuweka  utaratibu  wake  kwa  ajili  ya  kuongeza  madawati  lakini  pia miundombinu ya vyumba vya madarasa ili watoto wetu ambao sasa tumebaini kuwa   wamekuwa  wengi   waweze   kupata      mahali   pa   kukaa   na   chumba ambacho wanaweza kupata taaluma yao. Lakini hatuzuii mlipakodi yeyote wa sekta  nyingine  kuchangia  kujenga  madarasa  kwa  haraka  ili  watoto  wetu waingie  ndani,  kutoa  madawati  kama  ambavyo  tumeona  Watanzania  wengi 
wamejitokeza,  makampuni  mengi  yanachangia  lakini  pia  hata  baadhi ya Wabunge  tumeona  mkitoa  mchango  wenu,  na  mimi  nataka  nitumie  nafasi  hii kuwapongeza sana Wabunge ambao pia mmeanza kuunga mkono jitihada za Serikali kuchangia madawati.  Jambo hili ni letu  sote, watoto  ni wetu  sote hebu twende  pamoja,  tutoe  elimu  hiyo  ya kuchangia  kwa  namna  mtu  anavyoweza kwenye  madawati,  kama  una  uwezo  wa  kujenga  chumba  cha  darasa  ili watoto  wetu  waweze  kusoma  ndani,  lakini  Serikali  inaendelea  na  mkakati  pia 
wa ujenzi wa maeneo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa  Spika,  kwa  hiyo,  ningependa  nitamke  hili  ili  wale  wote wanaodhani  kulundikana  kwa  watoto  sasa  ni  jambo  la  makusudi,  hapana,  ni jambo  ambalo  tuliona  ni  muhimu  tupunguze  michango,  lakini  Wazazi  ambao walikuwa    wanashindwa    kuleta    watoto    nao    wapate    kupeleka    watoto, wamepeleka  watoto  wengi  ni  jukumu  letu  sasa  kujenga  vyumba  na  kupeleka madawati. (Makofi
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved