Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 3 | Sitting 49 | Works, Transport and Communication | Maswali kwa Waziri Mkuu | 1 | 2016-06-23 | 
 
									Name
Venance Methusalah Mwamoto
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Primary Question
						MHE.  VENANCE  M.  MWAMOTO:
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  ahsante  kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa Serikali ya utawala wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ilitimiza malengo yake ya kusaidia kupigania uhuru nchi za Afrika na hivyo kupelekea nchi zote kupata uhuru; nchi hizo wakati zikiwa hapa zilijenga  makambi  ambayo  yalitumika  kwa  ajili  yao  katika  sehemu  tofauti;  na kwa  kuwa  makambi  hayo  yametumika  baada  ya  kuondoka  kama  Vyuo  na Sekondari  na  pia  kufanya  wao  waendelee  kukumbuka  kwa  yale  ambayo tumeenzi:-
Ni  lini  Serikali  sasa,  itabadilisha  makambi  ya  wapigania  uhuru  hawa ambayo  yametumika  kama  Magereza  na  matumizi  mengine  yasiyofaa,  ili waendelee  kukumbuka  sehemu  ambazo  walikaa  kwa  ajili  ya  kupigania  uhuru wetu? 
					
 
									Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
						WAZIRI  MKUU:
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  naomba  kujibu  swali  la  kwanza kabisa la Mheshimiwa Mwamoto, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  ni kweli  kabisa  kwamba  nchi  yetu  ilishiriki  sana kuwakaribisha wapigania uhuru wa nchi mbalimbali, kuendesha harakati zao za kisiasa  hapa  nchini.  Maeneo  yote  waliyokuwa  wamekaa,  waliweza  kujenga miundombinu  mbalimbali  na  yanatambulika  kama  makambi  ya  wapigania uhuru. 
Katika   kumbukumbu   zangu,   Morogoro   kuna   eneo   linaitwa   Dakawa ambalo   sisi   tunatumia   kama   Sekondari,   lakini   pia   Mazimbu   pale   kwenye Compus ya SUA na  maeneo  mengine,  nakumbuka  kule  Nachingwea  kuna eneo  la  Matekwe  na  eneo  lile  lililotumika  ni  kama  vile  Pashule;  na  kuna  eneo pale  Msata,  hapa  jirani  Chalinze  pale  ambako  jeshi  linatumia  sana  kama sehemu  ya  mazoezi.  Pia  kuna  makambi  mengine,  nakumbuka  nikiwa  Naibu Waziri nilikuja kwako Kilolo, eneo moja kati  ya maeneo  ya makambi pale Kilolo ndiyo wanatumia kama Magereza.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa maeneo haya baada ya kuwa shughuli za wapigania    uhuru    kumaliza    kazi    zao,    Serikali    ilifanya    maamuzi    kutumia miundombinu ile kwa shughuli mbalimbali ikiwemo elimu. Eneo lingine kama hilo la  Msata,  Jeshi  na  pale  Kilolo,  Magereza.  Maeneo  hayo  yote,  kutokana  na nature ya  miundombinu  iliyopo,  maamuzi  haya  yalifanywa  ili  kutumia  kwa umuhimu  wa  mahitaji  ya  nchi.  Kwa  hiyo  basi,  eneo  kama  Kilolo  ambalo 
limetumika   kama   Magereza,   suala   la   Magereza   siyo   suala   la   matumizi yasiyokuwa muhimu, ni muhimu pia kwa sababu ni sisi wenyewe ndio tunaenda kuishi pale na ni maeneo ya mafunzo, lakini pia ni eneo ambalo tunawahifadhi wale ambao wamepatikana na hatia kadhaa na kwenda kutunzwa.
Mheshimiwa    Naibu    Spika,    kwa    hiyo,    pale    ambako    tumetumia miundombinu  ile  kwa  shughuli  nyingine  nje  ya  elimu,  basi  napenda  kutumia nafasi   hii   kuwasihi   Halmashauri   za   Wilaya,   pamoja   na   wananchi   kujenga miundombinu  mingine  kwa  ajili  ya  kutumia  kwa  matumizi  ya  elimu  na  haya maeneo   mengine   yanayotumika   kwa   elimu   yataendelea   kutumika   kama ambavyo imepangwa. 
Mheshimiwa  Naibu    Spika,  kwa  kumbukumbu  hizi    sasa  ukiangalia  kwa sehemu  kubwa,  makambi  yale  yote  yaliyotumika,  mengi  sana  yanatumika  ni kwa  matumizi  ya  elimu  zaidi  na  maeneo  machache  ndiyo  kama  hayo  mawili niliyoyataja, kule Msata na Kilolo ndipo ambako yanatumika kwa Jeshi  pamoja na  Magereza.  Yote  haya  ni  mambo  muhimu  kwetu  sisi,  ni  lazima  tutumie miundombinu  ile  ili  pia  badala  ya  kuwa  tumeyaacha  tu,  bora  yatumike  ili huduma mbalimbali ziweze kutolewa katika maeneo hayo.
					
 
											Name
Venance Methusalah Mwamoto
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Question 1
MHE.  VENANCE  M.  MWAMOTO:
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu mazuri, lakini nilikuwa naomba ile sehemu kwa  umuhimu  uliopo,  kwa  kuwa  wenzetu  wanaweza  kuja  siku  moja  pale,  kwa ajili ya 
kutaka kujua walipoishi; kwa kuwa ni sehemu ambayo ina kumbukumbu 
muhimu  na  viongozi  wengi  wakubwa  walikaa,  basi  angalau  Serikali  ifikirie kujenga  kitu  kingine  mbadala  kwa  ajili  ya  kuwaenzi  na  kuwakumbuka  wale wenzetu wa Afrika Kusini. Ahsante. 
 
											Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
								WAZIRI  MKUU:
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  Mheshimiwa  Mbunge  ametoa ombi  kwamba  kwa  kuwa  eneo  hilo  la  Kilolo  lina  umuhimu  wa  kuwa  na  shule nyingi  za  sekondari,  ifikiriwe  kuwa  eneo  hilo  libadilishwe  badala  ya  Magereza
liwe elimu. Ni wazo zuri na ni ombi,  tunaweza kuangalia ndani ya Serikali, lakini bado nilipokuwa najibu swali la msingi, nilisema eneo hilo la Kilolo linahitaji kuwa na taasisi za shule nyingi kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo. 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  bado  Halmashauri  na  wananchi  wanahitajika 
kuweka  mikakati  ya  ujenzi  wa  shule  nyingine,  huku  Serikali  ikiangalia  umuhimu na uwezekano wa kubadilisha hilo Gereza kuwa elimu; lakini bado Magereza ni eneo muhimu na ni jambo la msingi pia kuwa na Gereza kwenye eneo hilo. 
Mheshimiwa Naibu Spika,  kwa kadiri ambavyo Serikali tutafanya mapitio, 
tutaweza kuwapa taarifa wananchi wote wa Kilolo .
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved