Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 3 | Sitting 49 | Finance and Planning | Maswali kwa Waziri Mkuu | 2 | 2016-06-23 | 
 
									Name
Hamida Mohamedi Abdallah
Gender
Female
Party
CCM
Constituent
Lindi Mjini
Primary Question
						MHE.  HAMIDA  M.  ABDALLAH:
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  nakushukuru  kwa kunipa nafasi, lakini sasa nielekeze swali langu kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  ili  kuhakikisha  kuwa  Serikali  inatekeleza  lengo lake  la  sera  za  fedha  na  sheria  kwa  kupeleka  maendeleo  vijijini  na  hasa  kwa kuwapelekea  fedha  za  miradi  ya  maendeleo.  Je,  Serikali  ina  mkakati  gani  wa kuhakikisha  fedha  za  miradi  ya  maendeleo,  zinafika  katika  Halmashauri  kwa wakati ili kuhakikisha wanatekeleza shughuli za maendeleo? 
					
 
									Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
						WAZIRI    MKUU:
Mheshimiwa    Naibu    Spika,    naomba    nijibu    swali    la Mheshimiwa Hamida Mohamed Abdallah Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  ni  kweli  kwamba  Serikali  imeweka  nia  ya  dhati ya  kupeleka  fedha  zilizotengwa  kwa  ajili  ya  maendeleo  kwenye  Halmashauri zetu,  Wizara  na  Taasisi  za  Umma  ili  kufanya  kazi  za  maendeleo.  Waheshimiwa Wabunge   ni   mashahidi,   mwaka   huu   kupitia   bajeti   yetu   hii   ambayo   sasa tunaendelea nayo, tumefanya mabadiliko makubwa ya kutenga na kuongeza kiwango  cha  fedha  za  maendeleo  kutoka  asilimia  27  mpaka  asilimia  40. 
Malengo  yetu  ni  kuhakikisha  kwamba  miradi  yote  ya  maendeleo,  yale  yote ambayo   tunahitaji   yafanyiwe   maboresho,   yanatekelezwa   kama   ambavyo imekusudiwa.
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  Serikali  imeweka  mikakati  kadhaa,  moja ni kuhakikisha kwamba tunaongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato, lakini pia tunadhibiti  mianya  ya  ukwepaji  kodi  ili  kuweza  kujiongezea  pato  zaidi,  lakini kubwa  zaidi  ni  kusimamia  fedha  hizi  ambazo  tunazipeleka  kwenye  Taasisi  za Umma kwamba zinatumika kama ilivyokusudiwa. 
(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Serikali bado tunaendelea kuwataka watumishi, pindi fedha hizi zitakapokusanywa na baada ya Bunge hili, tutaanza kupeleka fedha kwenye mamlaka zetu za Serikali za Mitaa na Taasisi na Wizara. 
Nataka   nitumie   nafasi   hii   kuwaambia   Watumishi   wa   Umma   waliopewa dhamana  ya  kupokea  fedha  na  kusimamia  matumizi,  kuhakikisha  kwamba fedha  hii  iliyotengwa  inatumika  kama  ambavyo  imekusudiwa;  na  kwamba hatutasita  kuchukua  hatua  kali  kwa  yeyote  ambaye  atathibitika  kupoteza fedha hizi nje ya matumizi ambayo tumeyakadiria.
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  kwa  hiyo,  ni  mkakati  wetu  pia  kuhakikisha kwamba  baada  ya  makusanyo  tuzipeleke  fedha  zote.  Wajibu  mwingine  ni kuhakikisha  kwamba  miradi  inayotekelezwa  inakuwa  na  thamani ya  fedha iliyopelekwa   kwa   ajili   ya   matumizi   ya   maeneo   hayo.   Kwa   hiyo,   nataka niwahakikishie  Waheshimiwa  Wabunge  kwamba  Serikali  itasimamia  jambo  hili, lakini  pia  tushirikiane  Wabunge  wote,  nyie  pia  ni  Wajumbe  wa  Mabaraza  ya Madiwani  kwenye  maeneo  yenu.  Kwa  hiyo,  tusaidiane  tukishirikiana,  mkakati wa  Serikali  wa  kupeleka  fedha  kwa  wakati  na  mkakati  wa  Serikali  wa  kutaka 
kuongeza  fedha  ili  kupeleka  kwenye  maendeleo  uweze  kufikiwa  na  hatimaye Watanzania waweze kuiona tija. 
					
 
											Name
Hamida Mohamedi Abdallah
Gender
Female
Party
CCM
Constituent
Lindi Mjini
Question 1
MHE.  HAMIDA  M.  ABDALLAH: 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  namshukuru  sana Mheshimiwa  Waziri  Mkuu,  kwa  majibu  yake  mazuri,  lakini  ningependa  kujua sasa, eneo hili la watumishi kupitia Halmashauri zetu, wamejipangaje kwa suala zima la mapo
keo haya ya mabadiliko ya kuendelea kutaka kuleta maendeleo zaidi?  Kwa  sababu  kuna  maeneo  mengine  tuna  Makaimu  Wakurugenzi  na Makaimu  Watendaji  mbalimbali.  Sasa  napenda  kujua  Serikali  imejipanga  vipi katika eneo hili la Watendaji wetu? Ahsante. 
 
											Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
								WAZIRI MKUU:
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa namna gani tumejipanga kuhakikisha   fedha   hizi   zinapokelewa   na   watu   stahiki,   kwa   maana   wenye 
mamlaka   kamili;   kama   ambavyo   mnajua,   Mheshimiwa   Rais   anaendelea kuunda  Serikali  kwa  kuteua  watumishi  mbalimbali  katika  kada  mbalimbali. 
Najua  hatua  iliyobaki  sasa  ni  ya  Wakuu  wa  Wilaya  na  Wakurugenzi  wenye dhamana.  Wakurugenzi  watashirikiana  na  Wakuu  wa  Idara  na  watumishi  wote kwenye Halmashauri zetu.
Kwa  hiyo,  moja  kati  ya  mikakati  ya  kuhakikisha  kwamba  tunapeleka 
fedha  kwa  wahusika  ni  kwa  kukamilisha  uundaji  wa  Serikali  kwenye  ngazi  ya mamlaka ya Serikali za Mitaa na Halmashauri za Wilaya jambo ambalo litatokea pindi  Mheshimiwa  Rais  atakapofanya  maamuzi  ya  kusoma  orodha  ya  Wakuu wa Wilaya na Wakarugenzi.
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  muhimu  zaidi,  ni  kwamba  mtumishi  yeyote 
atakayekuwa kwenye eneo hilo na fedha zimefika na anawajibika kuzipokea ili aende kuzisimamia, anao wajibu wa kuzisimamia. Kwa sababu jukumu hili la kila mtumishi wa mamlaka ya Serikali za Mitaa, inaweza kuwa Mkurugenzi au Mkuu wa Idara na Mkuu wa Idara huyo kwa idara yake, anawajibika kupeleka fedha kwenye ngazi ya vijiji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi anawajibika kufanya hilo na  Serikali  haitasita  kuchukua  hatua  kali  kwa  yeyote  ambaye  atahusika  kwa ubadhirifu  wa  fedha  ambazo  tutazipeleka  kwenye  shughuli  za  maendeleo kwenye ngazi zetu za Vijiji na Kata. 
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved