Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 3 | Sitting 49 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Maswali kwa Waziri Mkuu | 3 | 2016-06-23 | 
 
									Name
Richard Phillip Mbogo
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Nsimbo
Primary Question
						MHE.  RICHARD  P.  MBOGO:
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  nakushukuru  kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara  ya  Elimu,  Sayansi  na  Teknolojia,  ina  sera  nzuri,  ina  sheria  mbalimbali  juu ya   elimu   ambazo   zinapelekea   wanafunzi   wa   Kidato   cha   Nne   waliofaulu, wanachaguliwa   na   kwenda   Kidato   cha   Tano.   Mara   nyingi   kwa   maarufu 
wamesema huwa kunakuwa na selection.
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  kwa  kuwa  kuna  habari  ambazo  zinazagaa kwamba  mwaka  huu  Serikali  haitachukua  wanafunzi  kutokana  na  sababu ambazo  bado  hazijaeleweka.  Sasa  je,  Mheshimiwa  Waziri  Mkuu,  jambo  hili  lina ukweli gani? Kama lipo, Serikali inatoa kauli gani juu ya suala hilo? 
					
 
									Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
						WAZIRI   MKUU:
Mheshimiwa   Naibu   Spika,   naomba   kujibu   swali   la Mheshimiwa Mbogo, Mbunge wa Nsimbo kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  kwanza  nataka  nikanushe  kwamba  Serikali haina   mpango   wa   kuwapanga   vijana   wetu   waliomaliza   Kidato   cha   Nne kwenda  Kidato  cha  Tano.  Najua  tuna  makundi  mengi  ya  watu  wanapenda kupotosha   tu   habari,   ikiwemo   na   hii,   lakin
i   nataka   nitumie   nafasi   hii kuwahakikishia  wanafunzi  wote  waliomaliza  Kidato  cha  Nne,  wanaopaswa kwenda  Kidato  cha  Tano,  lakini  na  wazazi  pia  wa  vijana  wetu  hawa  kwamba Wizara  ya  TAMISEMI  yenye  dhamana  na  Sekondari,  kwa  pamoja  na  Wizara  ya 
Elimu,  kazi  ya  upangaji  wa  vijana  wanaokwenda  Kidato  cha  Tano  inaendelea na  wakati  wowote  ule  mwishoni  mwa  mwezi  huu  majina  hayo  yatakuwa yametoka. 
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi zinazofanywa sasa, nyie wote mnatambua kwamba mwaka uliopita wanafunzi hawa walikuwa wanapangwa kwa mfumo wa GPA na  sasa  tumebadilisha 
GPA kwenda division.  Kwa  hiyo,  kazi  ambayo Wizara  ilikuwa  inafanya  ni  kubadilisha  ule  mfumo  wa GPA kwenda division ili uweze kuwapanga vizuri kwa division zao na sifa ambazo zinatakiwa. 
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la upangaji halikuwa ni kwa ajili ya Kidato cha Tano peke yake, kuna wale ambao tunawapeleka Vyuo kama Afya, Kilimo na maeneo mengine, nao pia wanatakiwa wapangwe kwa mfumo wa division na wote hao unapowapanga Kidato cha Tano, ili wengine waweze kupangwa, zoezi hili lazima lifanywe kwa pamoja. 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  kwa  hiyo,  kazi  hii  inakamilika,  itatoka  muda mfupi  ujao  na  kwa  hiyo,  baada  ya  hapo  Serikali  itatoa  majibu  haya  wiki  mbili kabla  ili  kuwawezesha  wazazi  kujipanga  vizuri  kuwapeleka  vijana  wao  kwenye maeneo mengine.
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  pia  kulikuwa  na  kazi  ya  sensa  ya  kuhakikisha tuna  shule  ngapi  za  Kidato  cha  Tano  ili  tuweze  kuwapeleka  vijana  wetu  wote. 
Kwa  sababu  mwaka  huu  ufaulu  ni  mkubwa  zaidi,  kuliko  mwaka  jana,  2015.
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  kwa  hiyo,  lazima  tuhakikishe  tunawapeleka vijana  kulingana  na  uwezo  wa  shule  ili  tujue  tumewapeleka  wangapi  na wanaobaki  wangapi  wenye  stahili  ya  kwenda  Kidato  cha  Tano  ili  nao  wapate nafasi  ya  kupangiwa  maeneo mengine  kwa  stahili  ile  ile  ya  Kidato  cha  Tano  ili waziweze  kupoteza  ile  stahili  yao  waliyokuwanayo  ya  Kidato  cha  Tano;  kama vile  kuwapeleka  kwenye course za  miaka  mitatu  za Diploma ambapo  miaka miwili  huitumia  kwa  ngazi  ya  Kidato  cha  Tano  na  cha  Sita,  wakishafaulu 
wanaingia kwa profession, kama ni afya, kama ni kilimo, kama ni sekta nyingine; kwa mfano Ualimu, ili waweze kuendelea na stahili yao ya Kidato cha Sita. Kwa hiyo, kazi hiyo itakapokamilika, tutaweza kutoa taarifa mapema. 
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved