Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 3 | Sitting 49 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Maswali kwa Waziri Mkuu | 4 | 2016-06-23 | 
 
									Name
Cosato David Chumi
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Primary Question
						MHE.  COSATO  D.  CHUMI: 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  nakushukuru  kwa kunipa nafasi hii, nami niweze kumwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu swali ambalo nimeona  kuna  umuhimu  wa  kuliuliza  kwa  sababu  jana  nilisikia  ufafanuzi  kutoka kwa Mheshimiwa Rais, lakini bado nimeendelea kupokea 
message kutoka kwa watu mbalimbali wakiuliza kuhusu swali hilo. Suala hilo ni kwamba, kumekuwepo na  taarifa  katika  mitandao  ya  kijamii  na  mitaani  kwamba  Serikali  imefuta  ajira hali  ambayo  imesababisha  tahamaki  na  taharuki  miongozi  mwa  wahitimu mbalimbali waliokuwa wanatarajia kuajiriwa na Serikali. 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  pia,  taarifa  hizo  za  mitandaoni  na  mitaani zinasema  pia  kwamba  Serikali  haitafanya  tena promotion wala  kupandisha madaraja, hali ambayo pia inawafanya Watumishi wa Umma kwa namna fulani morali yao kushuka. 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  sasa  napenda  kusikia  ukweli  halisi  ni  upi  katika suala  hili.  Je,  ni  kweli  kwamba  Serikali  haitaajiri  tena?  Ni  kweli  haitapandisha madaraja tena? Nakushukuru. 
					
 
									Name
Kassim Majaliwa Majaliwa
Gender
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
						WAZIRI   MKUU: 
Mheshimiwa   Naibu   Spika,   naomba   kujibu   swali   la Mheshimiwa Cosato Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  kama  ambavyo  nimejibu  swali  la  Mheshimiwa Mbogo,  ni  kwamba  sasa  hivi  kuna  watu  wengi  hupenda  kusema  maneno ambayo siyo sahihi na hili pia napenda nikanushe.
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  kwa  bahati  nzuri  sana  Mheshimiwa  Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana kwenye hotuba yake ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya  Benki Kuu,  ametoa ufafanuzi mzuri sana.   Nami nataka nitumie nafasi   hii   kurudia   tu   yale   ambayo   Mheshimiwa   Rais   ameyasema   kwa kuwahakikishia  Watumishi  wa  Umma  na  wale  ambao  wanatarajia  kuajiriwa kwamba Serikali haijasitisha ajira. 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  Serikali  imesimamisha  kwa  muda  kuajiri  kwa sababu tunaendelea na zoezi la uhakiki wa watumishi hewa. Kazi hii ilishaanza, sasa  hivi  tunaikamilisha.  Katika  ukamilishaji  huu,  tunataka  tujue  sasa  watumishi hewa ni akina nani kwa kila idara na kila sekta na watumishi walioko sasa kazini ni  akina  nani;  ili  tuweze  kujua  idadi  ya  watumishi  waliobaki  na  pengo  yaliyopo ndipo sasa tuweze kuajiri kwa ajili ya kusheheneza mahitaji ya watumishi kwenye maeneo hayo. 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  pia  Serikali  inafanya  mapitio  ya  Miundo  ya Utumishi  kwa  lengo  la  kuboresha.  Tunaposema  kuboresha,  maana  yake  sasa tunataka tupate tija zaidi kwa watumishi. Kwa hiyo, naomba niwasihi Watumishi wote  wa  Umma  kwamba  zoezi  hili  halilengi  kuwakandamiza  watumishi;  kazi  hii hailengi kuathiri utumishi wao na madaraja yao, bali kuboresha watumishi. 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  nataka  niwahakikishie  Watumishi  wa  Umma kwamba  Serikali  hii  inawapenda  sana  na  inajali  mchango  mkubwa  ambao watumishi mnautoa  kwa Serikali h
ii. Ili tuweze kufanya kazi kwa motisha, Serikali hii  imeona  ni  muhimu  sasa  kuboresha  zaidi  miundo  mbalimbali  na  maslahi mbalimbali,   lakini   pia   kuona   idadi   ya   watumshi   tuweze   kutumia   fedha inayotakiwa. 
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka muwe na amani kwamba kazi hii inayoendelea ni ya muda mfupi sana. Itakapokamilika, ajira zote ikiwemo na elimu,   afya,   majeshi,   ambazo   pia   zilikuwa   tayari   zianze   karibuni,   zote zitarudishwa na watu watapelekwa kwenye vituo vya kazi kwenda kuanza kazi zao na madaraja mapya yatakuwa yameshatolewa. 
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved